header

nmb

nmb

Thursday, February 11, 2010

Sudan, Chad zamaliza uhasama

Rais Omar al- Bashir
SUDAN imesema kuwa ipo tayari kuresjesha mahusiano na nchi jirani yake ya Chad hivyo kuongeza matumaini ya kumalizika mgogoro katika Jimbo la Darfur.

Rais wa nchi hiyo, Bw. Omar al-Bashir alisema kuwa ziara ya Rais wa Chad, Bw.Idriss Deby ndiyo imeweka kando matatizo kati ya mataifa hayo mawili.

Rais Bashir yeye pamoja na Rais Deby wako pamoja kuahakikishia wananchi wa Chad na Sudan kuwa wamefungua ukurasa mpya katika tofauti na ugomvi kati ya mataifa hayo mawili.
Kuanzia leo, mapigano yetu ya kila siku yamebadilika na kuwa amani, usalama na utengamano kwa ajili ya manufaa ya watu wa mataifa yote mawili,"alisema.

Vilevile kiongozi huyo alitangaza mpango wa pamoja wa maendeleo ya kudumu katika mpaka baina ya Chad na Sudan.

Kabla ya tangazo hilo la jana mwezi uliopita nchi hizo mbili zilikubaliana kuanzisha doria ya pamoja katika maeneo ya mpakani mwa nchi hizo mbili ili kuwaondoa waasi waliopo katika mpaka huo.

Kwa upande wake Rais Deby alitoa wito kwa waasi wa Chad kuweka silaha zao chini na akawahakikishia usalama endapo watarejea nchini Chad na kuondoka Sudan.

Nitawahakikishia hali ya usalama endapo mtarejea nyumbani kwenu na kujiunga na shughuli za kijamii,"alisema Rais Deby.

Alimualika Rais Bashir ambaye anatafutwa na Mhakama ya Kimataifa inayoshughulikia Makosa ya Uhalifu wa Kivita ICC kwa tuhuma za uhalifu wa kivita katika Jimbo la Darfur ili akautembelee mji mkuu wa Chad, N'Djamena hivi karibuni.

Kiongozi huyo aliyataka makundi ya wapiganaji nchini Chad kushiriki katika uchaguzi utakaofanyika baadaye mwaka huu.

No comments:

Post a Comment