header

nmb

nmb

Saturday, February 13, 2010

MWANZA ZAKAMATWA RISASI 60 NA BUNDUKI 2


JESHI la limekamata bunduki mbili aina ya SMG zenye nambari TT 9770N na 1976561627 zikiwa na magazini yenye risasi 60 kila moja na bastolakatika matukio mawili tofauti.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Jamal Rwambo aliwaambia waandishi wa habari ofisini kwake kuwa bunduki hizo zilitelekezwa na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi zikiwa ndani ya begi katika pantoni ya MV Birj iliyokuwa ikitokea katika visiwa vya Maisome, Ntama kupitia Kome Mchangani kwenda jijini Mwanza.
Kamanda Rwambow alisema kuwa watu wawili hao waliokuwa wanasafiri katika pantoni hiyo, walitiliwa mashaka na baadhi ya wasafiri ambao walitoa taarifa Jeshi la Polisi ili waweze kuwakamata na kuongeza kuwa kutokana na hali hiyo walitelekeza begi hilo ndani ya pantoni hiyo.
Katika hatua nyingine, Kamanda Rwambow alisema kuwa bastola moja yenye Nambari 90444 iliokotwa katika Soko la Mitumba maeneo ya Mlango Mmoja jijini hapa nakuongeza kuwa ilikuwa imetengenezwa kienyeji.
Tukio la kutelekezwa kwa bunduki hizo mbili limekuja baada ya gazeti la Majira kuripoti kuwa watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wamehamia jijini Mwanza kutokana na kuogopa operesheni chakaza inayoendelea katika baadhi ya visiwa vilivyoko katika Ziwa Victoria.

No comments:

Post a Comment