header

nmb

nmb

Wednesday, February 3, 2010

Kuelekea Bondeni 2010.Tujikumbushe Fainali za kombe la dunia 2002

unamkumbuka mchezaji huyo alikuwa ni noma


*Brazil bingwa mara tano*

Senegal ilishangaza ulimwengu

MWAKA 2002, mashabiki kote duniani walishuhudia kwa mara nyingine tena fainali za kombe la dunia ambazo safari hii ziliandaliwa kwa pamoja na nchi za Korea Kusini na Japan.
Finali hizi zilikuwa ni za 17 toka kuanzishwa kwake mwaka 1930, zilianza kutimua vumbi Mei 31 hadi Juni 30, nchi hizo zilichaguliwa na FIFA kuandaa fainali hizo Mei 1996.

Mgogolo ulioibuka

Mgogolo uliojitikeza uliwahusu wenyeji wa fainali hizo Japan na Korea, pamoja na kuwa zilikubaliana kuandaa kwa pamoja lakini tatizo lilikuwa ni jina ambalo lingebatizwa fainali hizi.
FIFA ilipendekeza fainali hizi ziitwe Kombe la dunia "Japan-Korea" kwa kufuata mfumo wa herufi kwa kiingereza lakini Korea ikaona jina lake linakuwa la mwisho kutamkwa kwa hiyo ikapendekeza kutumia mfumo wa herufi wa kifaransa "Corée" na "Japon" kwa maana hiyo jina la Korea litaanza yaani "Korea-Japan".


Januari 5, 2001, Yasuhiko Endo, katibu mkuu wa kamati ya maandalizi, aliwataarifu Korea kuwa itabadili jina hilo katika tiketi zitakazouzwa Japan na kuwaachia Korea kazi ya kubatiza jina la fainali hizo na wao kubaki na jina la "(Japan/Korea)".
Hata hivyo, Shirikisho la soka nchini Korea (KFA) liliilalamikia FIFA kwa madai kuwa kitendo cha Japan kubadili jina hilo yaani 'Japan-Korea' badala ya Korea-Japan kungevuruga makubaliano yao.

FIFA ilikubali hoja hiyo na kuimaru Japan kuacha kubadili jina hilo, Japan iliamua kuondoa jina lake na kuziita fainali hizo 'kombe la dunia 2002' na kuondoa jina la "Korea/Japan".
Baada ya mgogolo huo FIFA iliamua kutoruhusu nchi zozote kuandaa fainali hizo kwa kushirikiana na azimio rasmi lilipita mwaka 2004.

*Timu zilizofuzu fainali hizo.

Takribani timu 199 zilikuwa zikiwania nafasi ya kushiriki fainali hizo, lakini ni timu 32 tu ndizo zlizofanikiwa huku mabingwa watetezi Ufaransa na wenyeji wa fainali hizo Korea na Japan zikifuzu moja kwa moja bila kucheza mechi za awali.

Hata hivyo, mfumo wa kumpitisha moja kwa moja bingwa mtetezi bila kucheza mechi za kufuzu, ulitumika kwa mara ya mwisho katika fainali hizi.

Mbali na hilo, jumla ya mataifa manne yalifuzu kwa mara ya kwanza kushiriki fainali hizo, mataifa hayo ni China, Ecuador, Senegal, na Slovenia.


Kabla ya fainali hizi, Desemba 1, 2001, FIFA ilikutana kwa ajili ya kupanga makundi ambapo kundi F lilionekana kuwa ni kundi la kifo kutokana na kuundwa na timu ngumu zikiwamo Argentina, England, Nigeria na Sweden.


*Mechi za makundi
*Kundi A

Wageni wa fainali hizo Senegal, waliushangaza ulimwengu baada ya kuwachapa mabingwa watetezi Ufaransa 1-0, katika mechi ya ufunguzi wa fainali hizo.
Mechi hiyo iliyochezwa Mei 31 katika uwanja wa Seoul nchini Korea, Senegal ilifunga goli lake kupitia kwa Boupa Diop dakika ya 30 ya mchezo huo.


Mabingwa hao watetezi walitolewa baada ya kutoka suluhu na Uruguay na baadaye kuchapwa 2-0 na Denmark. Katika kundi hili Denmark na Senegal zilifanikiwa kusonga mbele.

*Kundi B
Hispania ilikuwa kinara wa kundi hili baada ya kuzichapa Paraguay na Slovenia 3-1 kila moja na baadaye kuiuwa Afrika Kusini 3-2. Hispania na Paraguay zilisonga mbele na kuzitupa Slovenia na Afrika Kusini.


*Kundi C
Timu nyingine kushinda mechi zote ilikuwa ni Brazil iliyokuwa kundi C, iliungana na Uturuki kusonga mbele na kuzitupa Costa Rica naChina,iliyokuwa ikifundishwa na Bora Milutinović.


*Kundi D

Marekani nayo iliushangaza ulimwengu baada ya kuichapa Ureno 3-2 ambayo ilifungasha virago mapema pamoja na Poland huku Korea na Marekani zikisopnga mbele.
*Kundi EUjerumani iliifanyia mauaji Saudi Arabia baada ya kuichapa 8-0 katika kundi hili. Timu hiyo ilishika usukani wa kundi hilo ikifuatiwa na Ireland huku Cameroon na Saudi Arabia zikirudi nyumbani.


*Kundi F

Mshangao mwingine ulitokea katika kundi hili la kifo, waliowahi kuwa mabingwa wa kombe hilo Argentina walishindwa kusonga mbele baada ya kuchapwa na England 1-0 kwa penalti iliyopigwa na David Beckham.Sweden na England zilifuzu kundi hilo na kuziacha Nigeria na Argentina

*Kundi G.

Italia, Croatia, Mexico na Ecuador zilikuwa katika kundi hili, lakini ni Mexico na Italia ndizo zilizosonga mbele.

*Kundi H
Lilikuwa ndilo kundi dhaifu katika fainali hizi, Japan, Ubelgiji, Urusi na Tunisia ziliunda kundi hili. Ni Japan na Ubelgiji ndizo zilizosonga mbele.
Baada ya hatua ya makundi na mtoano kumalizika timu za Ujerumani, England, Hispania, Senegal, Marekani, Brazil,Korea na Uturuki.

Mechi zilizokuwa na msisimko zaidi katika hatua hii ni kati ya England na Brazil ambapo Ronaldinho wa Brazil alipiga mkwaju wa faulo uliompita kirahisi kipa David Seaman na kuibuka ushindi wa 2-1.

Katika mechi nyingine, Sweden ilichapwa na Senegal 2-1 baada ya kutofungana katika dakika 90, Henri Kamara alifunga goli la dhahabu dakika ya 104 kwa senegal na kusonga mbele, mchezaji huyo pia ndiye aliyefunga goli la kwanza dakika ya 37.

Hata hivyo Senegal ilikuja kutolewa na Uturuki kwa goli la dhahabu lililofingwa na İlhan Mansız dakika ya 94 na kukatisha safari ya wawakilishi hao wa Afrika katika fainali hizo.


*Nusu fainali

Ujerumani iliichapa Korea 1-0, bao hilo liliwekwa kimiani na Ballack ambaye baadaye alioneshwa kadi ya njano na kukosa mechi ya fainali.

Ronaldo alifunga goli lake la katika mechi ambayo Brazil, iliichapa Uturuki 1-0 na kutinga fainali.
Katika mechi ya kutafuta mshindi wa tatu Uturuki iliichapa Korea 3-2, magoli ya Uturuki yalifungwa na Hakan Sukur dakika ya kwanza na Ilhan dakika ya 13 na 32.

*Fainali

Mechi hii ilifanyika Juni 30 katika uwanja wa kimataifa wa Yokohama, Japan. Mechi hiyo ilihudhuriwa na mashabiki 69, 029 huku mwamuzi akiwa ni Pierluigi Collina wa Italia.

Magoli mawili yaliyofungwa na Ronaldo dhidi ya Ujerumani yaliifanya Brazil kuwa mabingwa mara tano wa fainali hizo, mshambuliaji huyo aliibuka kinara wa mabao baada ya kuweka kimyani mabao 8 na kunyakuwa zawadi ya 'Golden Boot' huku Oliver Kahn akishinda zawadi ya 'golden ball'.

*Kumbukumbu muhimu.
Fainali hizi zilikuwa ni za kwanza kufanyika barani Asia. Ufaransa iliweka rekodi ya kuwa bingwa mtetezi iliyofanya vibaya zaidi katika fainali za kombe la dunia.
Ilikuwa ni michuano ya kwanza kuandaliwa kwa ushirikiano wa nchi mbili Korea na Japan katika historia ya fainali hizo.

No comments:

Post a Comment