header

nmb

nmb

Sunday, January 24, 2010

FUNDIKIRA AUWAWA KWA KIPOGO DAR!!


Mtoto wa mjini Swetu Fundikira amefariki leo ktk hospitali ya Muhimbili baada ya kipigo kutoka kwa watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo eneo la Mwanamboka Kinondoni.
Mashuhuda wa kipigo hicho wamedai kuwa kimetokana na makosa ya usalama barabarani ambapo Marehemu Fundikira alidaiwa kuwachomekea watu hao waliodaiwa kukasirishwa na kumkimbiza na kisha kumkamata eneo la Mwanamboka akisubiri taa za kuongozea magari.
Inadaiwa walipofika walishuka na kuzunguka gari la Fundikira kisha kumuomba ashuke na kuanza kujibizana hali iliyopelekea ugomvi na Marehemu kuzidiwa nguvu kupelekea majeraha makubwa yaliyomsababishia kifo chake.
Wachacharikaji wa Blog hii ya Pr habari wanaendelea kuwasiliana na Kamanda kanda maalum ya DSM Bw. Suleiman Kova kupata undani wa tukio hilo. Tutaendelea kuwapa habari hizi za majonzi.
MUNGU AILAZE ROHO YAKE MAHALA PEMA PEPONI

No comments:

Post a Comment