header

nmb

nmb

Tuesday, July 26, 2011

Washindi Redd's Miss Kinondoni


Mshindi wa kwanza wa mashindano ya Redd's Miss Kinondoni, Stela Mbuge, katikati akiwa katika sura ya furaha muda mfupi baada ya kutangazwa kuwa mshindi, (kushoto) ni mshindi wa pili Husna HMaulisi na (kulia) ni mshindi wa tatu Hamisa Hassan. Fainali hizo zilifanyika juzi katika Ukumbi wa Mlimani City Dar es Salaam.

Stela aliibuka mshindi baada ya kuwashinda wenzake 11 baada ya kujibu vizuri maswali yaliyoulizwa na Miss Tanzania wa mwaka 2007, Richa Adhia.

Stela alizawadiwa sh. mil 2 pamoja na TV ya LCD iliyounganishwa na king'amuzi cha Star Time yenye thamani ya sh. mil 1.

Mshindi wa pili alikuwa Husna Maulid ambaye alizawadiwa sh. mil 1.5 na TV iliyounganishwa na King'amuzi cha Star Time, wa tatu alikuwa Hamisa Hassan ambaye alizawadiwa sh. mil 1.5 na tv iliyoungwa na King'amuzi.


No comments:

Post a Comment