header

nmb

nmb

Wednesday, September 8, 2010

WAFANYA BIASHARA WAGEUKA MAJIVU BAADA YA KUTEKETEA NA MOTO MANYARA!!



Na Waandishi Wetu, Manyara



WAFANYABIASHARA watatu wamekufa baada ya moto kuzuka ghafla wakiwa wamelala katika kibanda chao cha biashara



Kamanda wa Polisi mkoani humo, Parmenas Sumari, amesema tukio hilo limetokea jana usiku wakati wafanyabiashara hao wakiwa wamelala kenye vibanda vyao kwa nia ya kulinda mali.



Amesema wakati moto huo unaanza kuwaka wafanyabiashara hao hawakuweza kushtuka kutokana na kulala wakiwa fofofo.



Kamanda amesema waliokufa katika ajali hiyo wamefahamika kwa majina ya Mohamed Athuman (31), Abeid Idd (25) na mwenzao ambao wote ni wakazi wa mkoa wa Manyara.



Amesema tukio hilo ni la pili kutokea katika kipindi kifupi ambapo wiki iliyopita kulitokea ajali kama hiyo na kusababisha wafanyabiashara kufa na wengine kujeruhiwa.



Kamanda Sumari amewashauri wafanyabiashara kuacha kujiunganishia hovyo nyaya za umeme na kisha kulala ndani ya vibanda hivyo.



“Tunawashauri wafanyabiashara kama wanahitaji kulala kwenye vibanda vyao kwanza waandae mazingira mazuri na kisha waache tabia ya kuunganisha nyaya za umeme bila ya kufuata utaratibu,” amesema kamanda.



Amesema polisi inaendelea na uchunguzi wa tukio hilo ili kuweza kubaini chanzo cha ajali hiyo.

No comments:

Post a Comment