Na Mwandishi Wetu, jijini
KESHO Answari Sunna wanatarajia kusherehekea sikukuu ya Idd EL Fitri na kuwataka waislamu kutoa sadaka na pia kushiriki kwenye Uchaguzi Mkuu kwa kupiga kura.
Kiongozi wa Waanswari Sunna tawi la Tanzania Sheikhe Salim Sima amesema kuwa sikukuu hiyo itaswariwa kesho ama kesho kutwa kulingana na muandama wa mwezi.
“Kesho ndio tunatarajia iwe sikukuu yetu ambayo itakuwa Ramaadhani 29 mwaka 1431 Hijiria kama mwezi hautaandama itakuwa Ijumaa katika viwanja vya wazi,” amesema Sheikhe Sima.
Amesema Waislamu wanatakiwa kwenda kusali katika viwanja vya wazi ambavyo ni Mnazi Mmoja, Kidongo Chekundu, Mwembe Yanga, Mbagala Zakhiem, Mburahati Barafu, Gongo la Mboto na vingine.
Sheikhe Sima amesema katika kusherehekea sikukuu hiyo waislamu wanatakiwa wanatakiwa kutoa sadaka, kudumisha amani.
Pia amewataka Waislamu kutodanganyika na kuacha kushiriki kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 31 mwaka huu kutokana na kundi la baadhi ya watu wasipenda maendeleo.
“Kwa kuacha kushiriki uchaguzi au kufanya maandamano ni sawa na kumnyima mtu uhuru wake hivyo wasikubali kudanganyika,” amesema.
Hata hivyo, amesema wanaombea Uchaguzi Mkuu ufanyike kwa amani na utulivu bila ya kuwepo kwa uvujaji wa damu.
Mwisho…!
No comments:
Post a Comment