BENDI ya muziki wa dansi ya Kalunde ipo mbioni kuachia albamu yake ya pili hivi karibuni Dar es Salaam.Akizungumza Dar es Salaam jana, Rais wa bendi hiyo Deo Mwanambilimbi, alisema hadi sasa tayari wamekamilisha nyimbo mbili zitakazoingizwa katika albamu hiyo.
Alisema kwa sasa wapo studio kwa ajili ya kurekodi nyimbo hizo, ambazo zimeanza kurindima kuanzia jana katika kusherehekea siku kukuu ya Idi katika Ukumbi wa Giraffe Ocean View, Dar es Salaam.
Alizitaja nyimbo hizo kuwa ni Fungua iliyotungwa na Junior Gringo na Maiwane aliyoitunga yeye mwenyewe huku wakiendelea kuandaa nyimbo nyingine, ili kukamilisha albamu hiyo.
Mwanambilimbi alisema, albamu hiyo ni ya pili tangu kuanzishwa kwa bendi hiyo, ya kwanza ikijulikana kwa jina la Hilda ambayo iliweza kufanya vizuri katika tasnia ya muziki huo hadi kuingizwa tuzo za Kilimanjaro.
Alisema licha ya bendi yake kuanza kuwapa wapenzi wake nyimbo hizo, pia itaendelea kuwapagaisha na nyimbo zao za Hilda, Itumbangwewe, Nataka kuzaa na wewe, Usiniguse na Kilio kilio. Pix Habari kwa hisani ya Blog ya Burudan Mwanzo Mwisho
No comments:
Post a Comment