header

nmb

nmb

Tuesday, August 3, 2010

MWANAFUNZI CHUPUCHUPU KUJIUWA KISA MAISHA MAGUMU ATINGA MBELE YA HAKIMU!!

Baadhi ya wanafunzi wakiwa katika Semina.Kwa sasa imeibuka wimbi la kutaka kukatisha maisha yao


MWANAFUNZI wa kidato cha kwanza katika shule ya sekondari Malamba mawili Mbezi, Scolastika Uloga (16),mkazi wa Kigogo amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni kujibu shitaka la kujaribu kujiua na sumu ya panya.



Maelezo ya awali ya mwanafunzi ameiambia Mahakama kuwa, amechukua uamuzi wa kutaka kujiua kwa sababu dunia imemschosha na hata akiachiwa huru atajiua tu.



Mbele ya Hakimu Suzan Kihawa imedaiwa na Mwendesha Mashitaka Inspekta wa POlisi Nassoro Sisiwaya kuwa, Julai 17, mwaka huu, mshitakiwa alijaribu kujiua kwa kutumia sumu ya panya.



Mshitakiwa amekana mashitaka na kesi hiyo itatajwa tena Agosti 10, mwaka huu.
Pia,Endrew Charles (18),mkazi wa Kijitonyama amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni kujibu mashitaka ya wizi.



Mbele ya Hakimu Anipha Mwingira imedaiwa kuwa,Julai 23, mwaka huu, mshitakiwa aliiba pesa taslimu sh.5000 ambayo ilikuwa ni mali ya mlalamikaji Frank Mulle.



Mshitakiwa amekana mashitaka na kesi hiyo itatajwa tena Agosti 12, mwaka huu.
Pia, Jane Kayombo (24), mkazi wa Mwananyamala amefikishwa katika Mahakama ya Mwanzo Kinondoni kujibu mashitaka ya kutoa matusi hadharani.



Mbele ya Hakimu Anna Mshigwa imedaiwa na Karani Moses Mchome kuwa, Julai 25, mwaka huu,mshitakiwa alimtukana mlalamikaji Kaniz Khan.
Mshitakiwa amekana mashitaka na kesi hiyo itatajwa tena Agosti 10, mwaka huu.
By. Rehema Maigala wa Dar leo

No comments:

Post a Comment