Baadhi ya warembo wanaoshiriki katika shindano la Vodacom Miss Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja leo kwenye kambi yao iliyopo kwenye hoteli ya Giraffe Ocean View Mbezi Beach kwa muda wa siku 28. Shindano la Vodacom Miss Tanzania linatarajiwa kufanyika mwezi Septema 2010 jijini Dar es salaam katika kutafuta mrembo wa Tanzania ambaye atawakilisha nchi kwenye shindano la Miss World hapo baadae mwaka huu. Leo ilikuwa ni siku ambayo imepangwa mahsusi kwa ajili ya warembo hao kukutana na wanahabari na kuongea nao mambo mbalimbali yanayohusu maandalizi kwa ajili ya shindano hilo kubwa nchini na linalodhaminiwa na kampuni ya simu za mikononi ya Vodacom Tanzania.
No comments:
Post a Comment