TAARIFA YA KUZIMWA KWA MTAMBO WA RUVU JUU.
DAWASCO inawatangazia wateja wake kwamba mtambo wa kuzalisha maji wa Ruvu Juu utazimwa kwa saa 12.
TAREHE: 14.08.2010(Jumamosi)
SAA: 2:00 Asubuhi hadi 2:00 Jioni.
SABABU: Matengenezo ya miundombinu ya umeme wa kuendeshea mitambo ya kusukuma maji.
MAENEO YATAKAYOKOSA HUDUMA: Ni pamoja na Mlandizi, Kibaha, Kibamba, Mbezi, Kimara,Msewe Changanyikeni, Ubungo, Kibangu, Makuburi, Tabata, Kisukuru na maeneo ya jirani.
Tunawaomba wananchi wote wa maeneo hayo tuliyoyataja kuhifadhi maji kwa ajili ya kutumia katika kipindi ambacho mtambo utakua umezimwa.
Huduma ya maji itarejea katika hali ya kawaida ifikapo siku ya Jumapili.
DAWASCO inaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.
Isaidie DAWASCO kwa kulipa bili yako ya maji ya kila mwezi ili iweze kutoa huduma bora jijini.
Tutakufikia”
“
DAWASCO
No comments:
Post a Comment