Baadhi ya madenti waliolala barabarani kuzuia magari na Pikipiki isipite
TUMBO LA UDELE LINAUMA MMO!!
Dereva wa pikipiki anapo chezea Kichapo (mwenye fulana ya pundamilia) akipewa kichapo na akina mama baada ya kutaka kupita kinguvu eneo lililofungwa.
WAKAZI wa Kunduchi Mtongani jijini Dar es Salaam, jana walizua kizazaa baada ya kuifunga barabara kuu inayotoka Mbuyuni kuelekea eneo hilo kufuatia gari aina ya Toyota Hiace linalofanya shughuli za daladala kati ya Kunduchi na Mwenge kuwagonga na kuwaua watoto wawili wa familia moja.
Vurugu hizo zilisababisha askari wa kutuliza ghasia FFU, kutumia mabomu ya kutoa machozi ingawa baadaye walikatazwa kutumia mabomu hayo na askari wa JWTZ wa kambi iliyopo jirani na eneo hilo kutokana na muingiliano wa mionzi kati ya mabomu hayo na vifaa vyao. Picha kwa hisania ya global
No comments:
Post a Comment