header

nmb

nmb

Friday, June 11, 2010

MDAU MPANJI ATEMBELEA MAAJABU MAKUU YA TANZAZIA!!

Jiwe
Mdau akipozi kwa ajili ya kupiga pichas katika mto ambao una Daraja ra Mungu

Daraja lenyewe ni hili halikutiwa mkono na m2 ypyote isipokuwa Mungu

Hapa ni Daraja la Kisasa lililotengenezwa na Serikali yetu


Nimebahatika kufika katika daraja la Mungu lililopo Kiwira karibu na Chuo cha Magereza Kiwira,Wilaya ya Rungwe,mkoani Mbeya ambapo kwa muda niliofika majira ya saa 12 jioni palionekana ni sehemu ya kutisha na hasa baada ya kuteremka chini katika pango la daraja hilo ambako maji ya mto Kiwira yanapita na juu watembea kwa miguu wakipita,ni kivutio kizuri cha kitaalii na nikiwa napita kuelekea chini ya pango la daraja hilo nilipitishwa na wenyeji wetu akiewpo mtoto wa miaka 13 ambaye alinipitisha juu ya daraja hilo na kukuta jiwe (Bicon)la saruji lililojengewa na bomba likiwa limeandikwa 8-2-72 na namba T- 142 kama linavyoonekana katika picha tofauti juu ya daraja la mungu na kwa mujibu wa wenyeji hao hapo dipo walipoweka alama wazungu baada ya mzungu mwenzao haikujulikana ni raia wa wapi kupotelea katika maporomoko ya maji kama yanavyoonekana katika picha tofauti. Kwa mujibu wa wenyeji wa maeneo hayo raia huyo wa kigeni inasemekana alifika na wenzake kwa lengo la kufanya utafiti katika maporomoko hayo baada ya kupata taarifa ambazo hazijathibitishwa hadi sasa kuwa katika maporomokohayo kuna dhahabu nyingi za ajabu lakini kuna nyoka mkubwa ambaye amelalalia madini hayo ya thamani hivyo raia hao wa kigeni wanadaiwa walimfunga mwenzao minyororo na kutumbukia katika maporomoko hayo kwa lengo la kufuatilia ukweli lakini baada ya masaa kadhaa walipovuta mnyororo ulirudi peke yake bila mzungu hadi kesho. Kwa mujibu wa wenyeji wazungu hao wamekuwa wakifika kila mwaka na kupiga picha katika jiwe hilo lililopo juu ya daraja la mungu .Mwandishi, Thompson Mpanji kutoka Mbeya.

No comments:

Post a Comment