header

nmb

nmb

Thursday, April 1, 2010

MSAADA !!! ASANTENI WACHINA..IMEANDALIWA NA OFISA HABARI WA WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII BI. CATHERINE SUNGURA


Gavana Sun Liang akiagana na mwenyeji wake waziri wa afya na ustawi wa jamii mara baada ya mazungumzo mafupi yaliyofanyika kwenye ukumbi wa wizara hiyo.
Gavana wa Jimbo la Zhangdong nchini China Bw.Sun Liang akizungumza na waziri wa afya na ustawi wa jamii Profesa David Mwakyusa ( hayupo pichani) kwenye ukumbi wa wizara hiyo mara baada ya kuwasili n hapa nchini, ugeni huo upo hapa nchini ambapo wachina wamejitolea kujenga kituo cha kutibu magonjwa ya moyo na upasuaji katika Hospitali ya taifa ya Muhimbili.
HABARI
Malalamiko yanayojitokeza mara kwa mara kuhusu huduma ambazo hazirizishi katika sekta za Afya zinazotolewa zikiwemo za uuguzi karibu mikoa yote hapa nchini ni dalili kuwa huduma inayotolewa inakabiliwa na changamoto nyingi.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya na Ustawi wa jamii Profesa David Mwakyusa katika mkutano wa kutoa taarifa kwa wadau juu ya utekelezaji wa mpango wa kuimarisha elimu ya maadili kwa wauguzi na wakunga nchini.

Profesa Mwakyusa alisema kuongezeka kwa malalamiko hayo katika sekta ya Afya inatokana na wauguzi kutumia kauli mbaya,lugha isiyofaa kwa wagonjwa pamoja na kutozingatia sheria na miongozo iliyowekwa ya uuguzi hivyo kupelekea ufanisi mdogo wa fani hiyo.

“Suala la maadili ni la kudumu hivyo kila wakati lazima lizungumziwe na liwe somo la kutahiniwa katika vyuo vyetu vyote vya wauguzi ili vijana wawe na msingi mzuri wa maadili na wakazane kulisoma kama masomo ya taaluma”.

Aidha aliwasihi wale wote waliopata mafunzo wawe chumvi itakayosambaa kila mahali na kutekeleza mikakati ili huduma za Afya ziwe za kuridhisha na kuboreshwa ili kuona malalamiko pamoja na vifo vinavyoepukika vinapungua.

“Katika kufikia malengo ya maendeleo ya milenia baadhi ya malaengo yanakwamishwa na ukiukwaji wa maadili unaofanywa na baadhi ya watendaji wenzetu, kwa kuzingatia kuwa wauguzi na wakunga ni asilimia 50 ya watoa huduma ni wajibu wenu kujituma na kutoa mchango katika kuinua hali ya afya na kuzuia vifo vinavyoweza kuepukika”malengo hayo hayatafikiwa ikiwa hakutakuwa na wauguzi waadilifu na wenye upole, aliongeza Mwakyusa.

Hata hivyo alisema serikali inaendelea kutoa hamasa kwa akina mama kujifungulia katika vituo vya Afya na kuwakinga akina mama na watoto na ugonjwa hatari wa malaria kwa kuwapatia hati punguzo za vyandarua vilivyowekwa dawa pamoja na kuongeza idadi ya wataalamu wa sekta ya afya na vituo vya kutolea huduma hadi katika ngazi za vijiji.

Jumla ya waauguzi na wakunga 304 toka kanda sita nchini ikiwemo Mbeya, Mtwara, Moshi,Morogoro, Dodoma na Mwanza wamepatiwa elimu ya maadili ya wauguzi na wakunga ambayo yanaratibiwa na Baraza la wauguzi na wakunga nchini na kufadhiliwa na mfuko wa uadilifu,uwajibikaji na uwazi,ofisi ya Rais sekretarieti ya maadili ya viongozi kwa umma nchini.

No comments:

Post a Comment