JIFUNZE KUPIKA HII
Jamani kila siku mambo mapya, na ndio raha ya maisha.Wengi kati yetu tunafahamu supu za aina mbalimbali ila hii ya leo nimeipenda zaidi, na ndio maana nimeileta katika safu yetu ili tuzidi kubadilishana ujuzi.
Supu ya nyanya, ndio pishi letu la leo ambapo mahitaji yake ni nyanya kilo moja, vitunguu viwili, thomu kijiko cha chai, nyanya kopo vijiko viwili vya supu,vidonge vya supu viwili, chicken stock mbili ili uweze kupata supu ya lita moja.
Mahitaji mengine ni pamoja na siagi gramu 10,mafuta Ya Zaytuun vijiko vitatu vya supu, chumvi kiasi na pilipili manga ya unga kijiko cha chai.
Jinsi ya kuandaaKatakata vitunguu vidogo vidogo halafu weka mafuta ya zaitun na siagi katika sufuria, acha siagi iyayuke.
Halafu kaanga vitunguu na thomu hadi vigeuke rangi kidogo kisha weka nyanya zilizokatwakatwa ndogo ndogo na nyanya kopo halafu endelea kukoroga. Tumbukiza vidonge vya supu katika maji ya moto ya lita moja, halafu koroga kisha mimina katika sufuria ya mchanganyiko wa nyanya. Acha ichemke na funika ipikike kwa muda wa nusu saa, baada ya hapo ipua katika moto, acha ipoe kidogo, kisha tia katika mashine ya kusagia na usage vizuri.
Weka chumvi na pilipili manga, kisha rudisha katika sufuria ishike moto tena, ukimaliza hapo supu yako itakuwa tayari kwa kunywa.Imeandaliwa na Bi.Rabia wa Majira
No comments:
Post a Comment