header

nmb

nmb

Friday, March 19, 2010

PONGEZI MR MPINGA ILA TUNA MAONI YETU NA USHAURI

Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Mohamed Mpinga akiwa katika picha ya pamoja na Rais Mstaafu wa Marekani, G.W. Bush alipotembelea nchini.
Bush alikuwa ni mwenye furaha kupiga picha na Mpinga.
Naitwa Joseph Johnson ,wa Michocheni B, ni mdau mkubwa wa blog hii ya prhabari, Napenda kutoa pongezi zangu za dhati kwa kuteuliwa kwako Bw. Mpinga kuwa mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani na kumpongeza aliyeona kuwa wewe unafaa.
Nina maswalio yangu mawili kuhusu usalama Barabarani:-
1. Je? Umejipangaje Kupambana na Rushwa ya Barabarani hasa zile za Mikoani zinazo fanywa na Askari wako wa kikosi cha Usalama Barabarani japo si kwa kuzimaliza ila kuzipunguza kwa kiasi kikubwa.
2. Je? Kamanda utajitahidi vipi kudhibiti waendesha Pikipiki za Kichina ambazo kwa sasa zimeenea nchi nzima na zimesha waachia watu wengi ulemavu wa kudumu na wa mpito kwa madereva na abiria wake.
Naomba majibu kupitia Blog hii Ahsante.

Naitwa Merry Sharon wa UK . Naanza kwa kukupongeza kwa kuteuliwa kushika wadhifa huo mkubwa wa kitaifa.
Sisi tulioko huku nje ya nchi huwa tunafarijika sana tukiona mambo huko nyumbani yanakwenda sawa.

Swali

1. Kamanda nimesoma makala yako imeeleza vizuri sana na kwamba mikakati ya jeshi lako kikosi chako ni mizuri ila je itatekelezeka Au ni siasatu?

2. Nimesoma, kuwa umeamua kuendesha jeshi hilo katika teknolojia ya Kisasa Je Umejipangaje kwa hawa wenye Magari wanao zidisha uzito na kwamba utawezaje kukoa elimu kwa abiria wanaoshushwa katika Mizani kuwasaidia wenye mabasi kukwepa Ushuru na Kuharibu miundo mbinu.

Mwaka juzi nilikuwa huko nyumbani na nilikuwa nikisafiri kutoka hapo DSM kwenda Mwanza kwa kweli njiani makondakta walikuwa wakitusumbua sana kila tulipokuwa tukifika katika mizani na ndio maana nimeuliza swali hilo.
Majibu kupitia blog hii ya prhabari.


Naitwa Papa Lukumba ni mtanzania ambaye kwa sasa naishi Afrika ya Kusini katika harakati za kusaka maisha Baba!!
Baba mimi nikutakie pongezi nyingi kwani kupiga picha na Buss hususani wakati ule alipokuwa Rais wa Marekani si kitu mchezo nakwamba hata yeye kuwaza na kuwazua kuona kuwa anastaili kukupongeza kwa kuongoza msafara wake kwa vizuri kweli si jambo rahisi kwa Rais mwenye majukumu ya kuiongoza Dunia kukukumbuka, Big Up kwa sana 2.
Sina swali ila nakukumbusha kuwa ni lazima uwe mkari kidogo na mpole kiasi la sivyo hao trafiki watakuchafuria kazi kwani ukiwaonea haya watakupanda hadi kichwani kwa rushwa.
UONGOZI wa prhabari.blogspot.com UNAPENDA KUWAPONGEZA WOTE WALIO TUMA MASWALI NA MAONI NA USHAURI KUPITIA prhabari@gmail.com KWA MDAU WETU KAMISHNA MPINGA TUKO PAMOJA WADAU KULIENDELEZA JAHAZI LA BLOG

No comments:

Post a Comment