header

nmb

nmb

Thursday, March 18, 2010

DUUUUUU NJEMBA HII NINOMA UKAME GANI HUU

Imeandikwa na Bi. Rehema Maigala, wa Gazeti la Dar Leo Pia inapatikana katika Gazeti hilo


MZAZI Frank Sekumbe (32), mkazi wa Makoka, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni kujibu mashitaka ya kumbaka mtoto wa kaka yake (9) na kumsabishia maumivu makali sehemu zake za siri.

Mbele ya Hakimu Sundi Fimbo imedaiwa na Mwendesha Mashitaka Inspekta wa Polisi Nassoro Sisiwaya kuwa, Februari 23, mwaka huu, mshitakiwa alimbaka mtoto huyo.

Mshitakiwa amekana mashitaka na kesi hiyo itatajwa tena Machi 30, mwaka huu.
BASI LA KUBEBA WATUHUMIWA LIKIWA LIMESHEHENI WATUHUMIWA HAO NA NDUGU WAKIWA CHINI WAKITAKA KUWA SABAHI NA KUWAPA POLE

KWA WAREVI TU


Imeandikwa na Godfrey Ismaely, wa Gazeti la Dar leo . Habari zaidi nunua DarLeo ya leo


MSHITAKIWA Hendry Ramadhan (20), mkazi wa Buguruni, amefikishwa katika Mahakama ya Mwanzo Buguruni kujibu mashitaka ya kuvunja baa na kuiba vinywaji.

Mbele ya hakimu Emmanuel Mbonamasabo, imedaiwa na karani Hyasinta Mambo kuwa Februari 24, mwaka huu, saa 7 usiku, Buguruni kwa Mkanda, mshitakiwa katika kosa la kwanza alivunja baa ya mlalamikaji Ephrahim Michael.

Katika mashitaka ya pili imedaiwa kuwa Februari 24, mwaka huu, saa 7 usiku, Buguruni kwa Mkanda, mshitakiwa, baada ya kufanikiwa kuvunja baa hiyo, aliiba bia kreti tatu, malta tatu na fedha tasilimu sh. 30,000, jumla ya mali zote zikiwa na thamani ya sh. 330,000.

Mshitakiwa amekana mashitaka na kesi yake itatajwa tena Machi 29, mwaka huu.yuko lumande kakosa dhamana

No comments:

Post a Comment