header

nmb

nmb

Monday, February 15, 2010

Waziri Mkuu Ukraine,Bi.Yulia-Tymoshenko

Waziri Mkuu Ukraine,Bi. Yulia-Tymoshenko
Matokeo ya uchaguzi wa rais Ukraine kupingwa
KIEV, Ukraine,

MGOMBEA aliyeshindwa katika uchaguzi wa rais nchini Ukraine, Waziri Mkuu Yulia Tymoshenko, ameahidi kupinga matokeo hayo mahakamani.

Akizungumza kwa mara ya kwanza tangu mgombea, Viktor Yanukovych atangazwe kuwa mshindi wa uchaguzi huo, Tymoshenko ameshutumu kuwepo kwa wizi wa kura na kusema kuwa mgombea huyo hakuchaguliwa kihalali.

Hata hivyo Bwana Yanukovych amemtaka mpinzani wake kuacha kupinga matokeo na ajiuzulu.

Ushindi wake ulikuwa ni mwembamba wa asilimia 3.48, na waangalizi wa kimataifa wamesema ni ishara njema ya kuonyesha demokrasia.

"Nataka kueleza kwa uwazi kuwa Yanukovych si rais wetu," amesema Tymoshenko katika matangazo ya moja kwa moja kwa njia ya televisheni.

"Lolote litakalotokea siku za mbele, kamwe hatakuwa rais aliyechaguliwa kihalali wa Ukraine." Aliongeza. BBC ripota

No comments:

Post a Comment