Walokole 'wakesha' ili Wachungaji wafufuke
* Watingisha majeneza ili kuwaamsha
* Watingisha majeneza ili kuwaamsha
NAIROBI, Kenya
WAUMINI kutoka sehemu mbalimbali za Kenya na wengine kutoka nchi jirani ya Uganda, juzi walikusanyika kwa kuimba nyimbo za kumtukuza Mungu na kufanya maombi ili utokee muujiza wa kufufuka kwa miili miwili ya watu waliokufa.
Watu hao waliokufa ni wachungaji wa kanisa la Kingdom Seekers Fellowship International ambao walifariki kutokana na ajali ya gari Jumatatu, waumini hao waliamini kwa kuomba sana Mungu anaweza kufanya muujiza kwa kuwafufua wapendwa wao.
Ajali hiyo ilitokea katika Barabara kuu ya Nairobi-Nakuru, waumini hao walikuwa wakiamini kuwa ajali hiyo ilikuwa ni kutokana na nguvu za shetani na muujiza ungeweza kufanyika kwa kuzishinda nguvu za giza.
“Wachungaji wetu wamekufa katika ajali barabarani ni muda wetu kumtisha shetani,ambaye amehusika na janga hili,” Mchungaji John Kamau William, ambaye ni mtendaji wa Kanisa alitangaza katika kusanyiko la watu nje ya kanisa lao mjini Nakuru.
Kulikuwa na umati mkubwa wa waumini na mashuhuda wengine waliofika ambao walikuwa wakitaka kushuhudia muujiza wa ufufuko ukifanyika.
Muujiza huo ulitarajiwa uwe wa kufufuka kwa wachungaji Patrick Wanjohi Wanja na Francis Kamau Ndetei ambao miili yao ilikuwa kwenye jeneza wakati huo.
Kwa hiyo, majeneza yalikuwa na miili ya wachungaji wawili waliofariki yalichukuliwa na kupelekwa kanisani, mbele ya kundi kubwa la waumini na waliokuwa wamezunguka na kuangalia ni kitu gani kitatokea.
Watu wengine wasiokuwa waumini walikuwa wamekusanyika hapo na kuwashangaa waumini waliokuwa bize kwa kuomba kwa sauti kubwa!
Kila mtu alijaribu kuomba kwa imani yake kwa sauti ya juu na kuna wakati lilitokea wingu la mvua na kuonekana kama mvua ingenyesha na muujiza kutimia.
Sara ziliendelea na kusali kwa nguvu zaidi lakini hakuna kilichotokea.
wachungaji wengi waliyazunguka majeneza na kuomba kwa nguvu kwa Mungu kwa zaidi ya saa moja.
Kuna wakati mke wa mchungaji, Ndetei alikwenda kwenye jeneza na kulishika na kumwomba Mungu kumwamsha mume wake.
Kuna kuumini mwingine alijaribu kulisukuma jeneza akitaka wachungaji kuamka kutoka katika 'usingizi mzito' lakini hakuna kilichotokea.
Hadi kufikia wakati huo, kulikuwa na wengine walioonekana kuwa na wasiwasi (imani haba) kama muuzija unaweza kutokea.
Ili kukomesha hisia kama hizo mchungaji, Apostle Steven Bulungi wa Uganda aliamua kuwafukuza watu waliokuwa na hisia kama za Thomaso.
Tomaso kwa mujibu wa Biblia mmmoja kati ya wafuasi wa Yesu ambaye alikuwa na imani haba, ambaye alitilisha kuhusu kufufuka kwa Yesu Baada ya kuambiwa hivyo alisema kuwa hataamini hadi amwone kwa macho na kushuhudia majeraha aliyopata kwa kupigiliwa misumari msalabani na kuchomwa mkuki.
Yesu alikuja kumtokea na kumtaka ashuhudie alichotaka kuona.
Mchungaji huyo alikuwa akipaza sauti kwa kuliambia kusanyiko la watu kuwa na imani inatosha na inaweza kutenda. Mnafanyia kazi maneno ya Mungu,” aliwatia hamasa waumini.
Kadiri muda ulivyokuwa ukienda waumini walianza kukata tamaa kwa kuona muujiza hautokei.
Baadaye Pasta mmoja alitangaza: “Miujiza mingine huwa haitokei hapo kwa hapo... Mbingu inajua kuwa tunataka kurudisha uhao wao,” alisema Pasta William .
Aliliambia kusanyiko la watu kwamba kama 'wapendwa wawili' hawatafufuka, ina maana kuwa wametimiza kazi yao duniani. Hata Yesu aliishi kwa miaka 33 tu, lakini alitimiza malengo yake duniani.
Pasta William alisema kuwa kama Ezekiel (Nabii katika agano la kale) alizungumza na mifupa na kurejea katika uhai, hata leo wakristo wanaweza kufanya hivyo.
“Muujiza ambao Mungu alifanya, kama tunavyosoma katika Biblia, inaweza kufanyika leo.”
"Ingawa muujiza haukutokea, waumini hawajaishiwa matumaini," aliongeza Pasta William
Ilielezwa kuwa kama wachungani hao wawili hawatafufuka hadi kufikia kesho, miili yao itazikwa.
*Habari hii imetafsiriwa na Deodatus Myonga kutoka Gazeti la Nation la Februari 23.
No comments:
Post a Comment