header

nmb

nmb

Thursday, February 25, 2010

HOFU YATANDA CUF KWA WAGOMBEA URAISI

SHEKE YAHAYA UTABIRI WAKE WAZUA HOFU KWA WAGOMBEA URAIS


HII NI PICHA YA JINI LITAKALO MTOA ROHO ATAKAYE SHINDANA NA JK KIKWETE

PFRO LIPUMBA ANAOGOPA KUUWAWA NA JINI

MWENYEKITI wa chama cha wananchi CUF Prof. Ibrahim Lipumba amesema ni mapema sana kwake kuweka wazi au kutangaza nia ya kugombea nafasi ya urais mwaka huu, kwa madai ya kuhofia kutimia kwa kauli za mtabiri maarufu wa nyota Afrika Mashariki na Kati Sheikh Yahya Hussein.

Prof. Lipumba alitoa kauli hiyo leo asubuhi wakati wa kipindi cha mahojiano 'Jambo Tanzania' kinachorushwa na Televisheni ya Taifa TBc 1, ambapo alidai kuwa kwa sasa hayuko tayari kuongea lolote juu ya nia yake ya kugombea ili kuepusha yasije kumtokea yaliyotabiriwa na mnajimu huyo maarufu nchini.

Alisema mchakato wa kumpata mgombea wa nafasi ya urais ndani ya chama chake unaendelea na kuwa utakapokuwa tayari na kwa muda muafaka basi chama chake kitaweka wazi, japo ameshindwa kuweka wazi kama atakuwa yeye au mtu mwingine.

"Tuna uhuru ndani ya chama na tunao watu wengi wenye uwezo wa kuongoza si lazima niwe mimi, mchakato wa kumpata mtu huyo unaendelea na wananchi wasubiri kupewa mgombea mwenye sifa, kama ni mimi au mtu mwingine itajulikana hapo baadaye" amesema Pro. Lipumba.

Amesema chama chake bado hakiridhishwi na jinsi ambavyoserikali ya CCM inavyoshugulikia matatizo ya wananchi hasa swala la kuwatoa katika umasikini, hivyo bado kunahaja ya wanachi kuwa na machaguo mbadala ya wagombea zaidi ya CCM peke yake.

Amesema pamoja na kuwa serikali ya awamu ya nne imeonesha nia na kujitahidi kushugulikia kero za siasa za Zanzibar hasa hili la serikali ya mseto, lakini bado kuna ukandamizwaji wa siasa za upinzani jambo linalowanyima fursa wanachi kupata viongozi wanaowataka.


Hivi karibuni Sheikh Yahya Husein alitabiri kuwa , yeyote atakayejitokeza kuwania nafasi ya urais kumpinga Rais Jakaya Kikwete kuwania nafasi ya urais ndani ya chama chake atakufa ghafla.

Kauli hiyo ilionekana kuwagusa viongozi mbalimbali na wanachama ndani ya CCM ambao walijitokeza kutoa maoni yao mbalimbali.



No comments:

Post a Comment