header

nmb

nmb

Friday, February 19, 2010

UKE WENZA NI BALAA...

Rehema Maigala,Kinondoni

Khadija Saidi (25), mkazi wa Mwananyamala, amefikishwa katika Mahakama ya Mwanzo Kinondoni kujibu shitaka la kumkata na wembe shingoni mke mwezake.

Ilidaiwa Mahakamani hapo kuwa mshitakiwa huyo alimkata mlalamikaji Christina Charles walipokuwa katika mziki wa taarabu 'rusha roho'.

Mbele ya Hakimu Mariamu Masamalo ilidaiwa na Karani Emakulatha Philipo kuwa Februari 15, mwaka huu, mshitakiwa alimkata na wembe mlalamikaji na kumsababishia maumivu makali katika mwili wake.

Mshitakiwa amekana shitaka hilo na yupo nje kwa dhamana mpaka kesi hiyo itakapotajwa tena Machi 3, mwaka huu.

Pia, Shariffa Athumani (19) na Aziza Waziri (17) wakazi wa Mwananyamala wamefikishwa katika Mahakama ya Mwanzo Kinondoni kujibu shitaka la kujeruhi.

Mbele ya Hakimu Mariamu Masamalo ilidaiwa na Karani Emakulatha Philipo kuwa, Februari 14 mwaka huu, mshitakiwa alimjeruhi Zuwena Hassan kwa kumkata na wembe.

Mshitakiwa amekana shitaka hilo na yupo nje kwa dhamana mpaka kesi hiyo itakapotajwa tena Machi 3 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment