Mlinzi wa AC Milan Mbrazil Thiago Silva (kushoto) akiwania mpira na mchezaji wa United Luis Antonio Valencia, wakati wa mechi ya ligi ya mabingwa hatua ya 16 iliyofanyika juzi katika uwanja wa San Siro mjini Milan. Manchester United ilishinda 3-2.
HABARI
MABINGWA watetezi wa ligi kuu ya nchini hapa Manchester United, itajitupa uwanjani Jumamosi hii kukwaruzana na Everton katika uwanja wa Goodson Park, mechi itakayochezwa saa 9:45 alasiri.
United itaingia uwanjani huku ikiwa na kumbukumbu ya kuichapa AC Milan 3-2 katika uwanja wa San Siro nchini Italia,katika mechi ya ligi ya mabingwa Ulaya.
Timu hiyo ambayo inashika nafasi ya pili ikiwa na pointi 57 nyuma ya vinara wa ligi hiyo Chelsea yenye pointi 58, itachuana na Everton inayoshika nafasi ya tisa, katika kusaka ponti tatu muhimu za ligi hiyo.
Katika mechi yao ya mwisho ya ligi, iliyochezwa Februari 10, United ilitoka sare na Aston Villa baada ya kufungana 1-1 katika uwanja wa Villa Park huku Everton nayo ikiichapa Chelsea 2-1.
United ikishinda mechi hii itafikisha pointi 60 lakini pia itategemea na matokeo ya Chelsea na Wolves, mechi itakayochezwa siku hiyo pia.
Chelsea itakuwa inakaribishwa na timu hiyo inayoshika nafasi ya sita kutoka chini ya msimamo wa ligi hiyo,katika uwanja wa Molineux, ili kujihakikishia nafasi ya kuendelea kufanya vizuri kileleni mwa ligi hiyo.
The Blues ilikuwa katika wakati mgumu Februari 10 baada ya kukubali kipigo cha 2-1 kutoka kwa Everton na kuwapunguza kasi ya kuwania taji la ligi hiyo.
Kwa kutumia fundisho hilo, Chelsea itaingia uwanjani kwa umakini mkubwa kuhakikisha haiaibiki tena mbele ya vibonde Wolves katika mechi itakayochezwa saa 12 jioni.
Katika mechi yao ya mwisho iliyochezwa Februari 10, Wolves iliichapa Tottenham 1-0 na kufikisha pointi 24 katika mechi 25 ilizocheza.
Ratiba kamili ya mechi hizo itakuwa kama ifuatavyo,
Jumamosi, Februari 20,2010
Arsenal v Sunderland, 12:00 jioni Everton v Man Utd, 9:45 alasiri Portsmouth v Stoke, 2:30 usiku West Ham v Hull, 12:00 Wolverhampton v Chelsea, 12:00
No comments:
Post a Comment