header

nmb

nmb

Monday, February 22, 2010

DAWASCO na mgao wa maji Kimara

Afisa mtendaji mkuu wa DAWASCO Mhandisi Alex Kaaya

Afisa mtendaji mkuu wa DAWASCO Mhandisi Alex Kaaya amewaambia wakazi wa Kimara Baruti kuwa watapata mgao wa maji mara mbili kwa wiki kama hakutakuwa na hitilafu itakayojitokeza kwenye mitambo kuanzia hivi sasa.
Akizungumza wakati wa kujibu maswali ya wananchi jana kufuatia malalamiko yaliyokuwepo katika eneo hilo hususani katika suala la maji Mhandisi Kaaya amewaambia wananchi hao kuwa upatikanaji wa maji ya kuaminika unategemea ukarabati wa mitambo na uboreshaji wa miundombinu na mabomba.
“Ninawaomba wananchi muelewe kwamba ili kutatua tatizo hili la maji inabidi mradi ambao unatekelezwa hivi sasa wa ukarabati wa mitambo kwa asilimia 100, uboreshaji wa miundombinu na mabomba kwa asilimia 95 na kupanua mtambo wa usambazaji wa maji kwa asilimia 95 ukamilike kabisa,” alisisitiza Kaaya.Hata hivyo Mhandisi
Kaaya amesisitiza kuwa suala la mgao wa maji ni lazima kutokana na ongezeko la watu katika jiji la Dar es Salaam ambalo linahitaji maji kwa wingi kuzidi uwezo wa vyanzo vya maji.Mpaka sasa maeneo yaliyofanyiwa matengenezo tayari yameshaanza kupata maji.
Maeneo hayo ni pamoja na Kimara kin’gongo,
Kimara temboni, maeneo ya Kilungule, Baruti pamoja na eneo lote la Msewe.Kaaya ameyataja maeneo ambayo hayajapata maji kuwa ni Golani, Bakery na Bonyokwa, hata hivyo Mhandisi huyo amesema jitihada ya kuyapatia maji maeneo hayo zinaendelea kufanyika.

No comments:

Post a Comment