TAARIFA KWA VYOMBO VYA
HABARI
Desemba 17, 2014
KUZINDULIWA KWA LADHA
NYINGINE MBILI ZA KINYWAJI CHA ZANZI CREAM
LIQUEUR - CHOCOLATE NA CAPPUCCINO
Kampuni ya Tanzania
Distilleries Limited wazalishaji wa bidhaa bora zaidi za vinywaji vikali na mvinyo
hapa nchini, leo inazindua ladha mbili nyingine za Zanzi Cream Liqueur. Ladha hizi ni Zanzi Chocolate na Zanzi Cappuccino.
Akizungumza na waandishi wa
habari jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi Mtendaji wa TDL, David Mgwassa,
alisema ana uhakika ladha hizi mbili za Zanzi Chocolate na Cappuccino zitapendwa
na wengi kwani utafiti ulifanyika wa muda mrefu kubaini ni ladha zipi zitafurahiwa
na watu wengi. Vile vile Zanzi Chocolate
na Cappuccino zimetengenezwa kwa kuzingatia ubora na viwango vya Kimataifa
katika kuzalisha wa bidha za Cream Liqueur.
Naye Meneja Bidhaa wa TDL,
Warda Kimaro alisema, “kauli mbiu ya Zanzi Cream Liqueur toka kuzinduliwa 2012
ilikuwa ‘Fursa ya Kujiliwaza’. Sasa
tunawapa wateja wetu fursa nyingine mbili za Kujiliwaza msimu huu wa sikukuu na
Zanzi Chocolate na Cappuccino.” Kimaro anawasihi watanzania kujaribu ladha hizo
mbili kwani ni za kipekee kwenye jamii ya cream liqueur hapa nchini.
Kinywaji cha Zanzi Cream
Liqueur kilizinduliwa 2012 na Tanzania Distilleries Ltd katika chupa zenye
ujazo wa 750ml na Pakiti zenye ujazo wa 100ml. June 2013, chupa za ujazo wa
200ml nazo pia zilizinduliwa na kuingizwa sokoni. August 2014, Zanzi Cream
Liqueur ilipata tuzo ya kimataifa ya ‘Double
Gold Award’ huko New York Marekani kutokana na ubora wake. Mafanikio ya Zanzi Cream Liqueur toka ilipozinduliwa
ndio yamehamasisha TDL kuzindua ladha ya Zanzi Chocolate na Cappuccino.
TDL inawatakia wateja wake
wote kheri ya Christmas na Mwaka Mpya na kuwasihi washereke na kujiliwaza na
Zanzi Chocolate na Zanzi Cappuccino msimu huu wa sikukuu.
-MWISHO-
Kuhusu SABMiller
SABMiller plc
moja kati ya makampuni makubwa ya bia duniani ikiwa na mikataba ya kutengeneza
na kusambaza bia kwenye nchi zaidi ya 60 katika mabara matano. Bia zake ni
pamoja na zile za kimataifa kama Miller Genuine Draft, Peroni Nastro Azzurro na
Pilsner Urquell vilevile na bia nyingine zinazoongoza kwenye masoko ya ndani ya
nchi mbalimbali. Nje ya Marekani, SABMiller ni moja ya kati ya makampuni
makubwa yanayotengeneza vinywaji vya Coca-Cola duniani. Hivi karibuni SABMiller
plc ilinunua kampuni ya bia ya Foster’s pamoja na shughuli zake za uzalishaji
nchini India.
SABMiller
imeorodheshwa kwenye masoko ya hisa ya London na Johannesburg.
No comments:
Post a Comment