Na Josephat Lukaza
Tasnia ya Filamu nchini imeanza kukua japo kwa mwendo wa kinyonga huku tukianza kuona baadhi ya wasanii katika tasnia hii wakianza kunufaika japo sio sana lakini tofauti na zamani. Leo Katika Filamu nitaongelea swala la Part 1 na 2 katika Filamu zetu za nyumbani.
Tasnia ya Filamu nchini imeanza kukua japo kwa mwendo wa kinyonga huku tukianza kuona baadhi ya wasanii katika tasnia hii wakianza kunufaika japo sio sana lakini tofauti na zamani. Leo Katika Filamu nitaongelea swala la Part 1 na 2 katika Filamu zetu za nyumbani.
Swala
la Part 1 na 2 hapa nchini imekuwa ndio fasheni kutokana na
watengenezaji, wasambazaji au wasanii wenyewe kuleta filamu ikiwa kwenye
part 1 na 2 huku kiukweli ikiwa ni wizi kwa Mtanzania ambae anaenda
kununua filamu hiyo, Mtanzania anaweza kuipenda filamu flani na akawa na
uwezo wa kuinunua hiyo hiyo moja lakini utakuwa filamu hiyo story yake
imekatwa mara mbili huku kipande cha pili kikiandikwa part 2 je huu sio
wizi?
Endapo
mtanzania huyu hatokuwa na pesa ya kununua part 2 maana yake ni kwamba
amedhulumiwa haki yake na wewe uliyeikata story na kuitengenesha kuwa
sehemu wakati story ni moja.
Ifikie
hatua Watanzania nao wajue kuwa Kununua Filamu yenye part 1 na 2 ni
wizi ambao wao wenyewe wanaibiwa kimacho macho na wafahamu kuwa Kununua
filamu ya part 1 na 2 ni kununua story moja kwenye DVD mbili. Ndio maana
tunasema Part 1 na 2 ni wizi kwa mtazamaji.
Filamu
za Part 1 na 2 ni filamu ambazo kwanza hazina ubora wa kimataifa
kwasababu ili filamu iweze kushinda tuzo labda nje ya nchi cha kwanza ni
Filamu hiyo kuwa na Ubora wa Picha, Story na vilevile iwe moja ambayo
story yake imekamilika.nk.
Leo
hii Tanzania ikitoka filamu ambayo haina part 1 na 2 basi watanzania
wachache ambao wanajua nini maana ya filamu ndio huweza kununua filamu
hiyo kwasababu filamu yenye Part 1 na 2 ukiiangalia Utakugundua kuwa
kuna baadhi ya vipande katika Filamu hizo havina umuhimu wa kuwepo
lakini vinawekwa ili kuongeza muda tu na kuifanya part 1 iwe ndefu
kidogo ili story iendelee part 2 VIpande hivyo ambavyo unaweza kukuta
havina ulazima wa kuwepo ni kama kipande ambacho kinaweza kumuonyesha
mshiriki wa filamu hiyo anatembea muda mrefu takribani dakika moja nzima
inamuonyesha anatembea au anafungua Geti, au watu wanaongea weee
kipande hikohiko kimoja sasa hii yote ni kwaajili ya Kujazia tu ili
wakate story iendelee part 2...
Inatakiwa
kufikia mahali sasa Watanzania tuinuke na tufungue macho sasa maana
kununua filamu yenye part 1 na 2 ni wizi tunaojitakia wenyewe kutokana
na kwamba tunakubali kununua story moja katika DVD Mbili.
Swala
la Part 1 na 2 imekuwa mtindo sasa kwa wasanii wetu kutoa story moja
ambayo ilitakiwa kuchukua lisaa limoja na dakika 20 basi Part 1 utaiona
inachukua dakika 50 huku vipande vya filamu hiyo vingi vikiwa havina
umuhimu wa kuwepo lakini msanii anaviweka ili kujazia muda tu katika
filamu yake huku part 2 ikiwa fupi.
Mfano
wa Filamu nyingi tu za Kitanzania ambazo zimeshinda tuzo huko marekani
ni filamu ambazo Hazina Part 2 ni Part 1 tu... Kutokana na Uhalisia kuwa
Ni vigumu sana kulibadilisha Soko lilivyo lakini Kampuni ya PRoin
Promotions imejivunia kuwa ni Kampuni ambayo imeshaanza kuleta
mabadiliko katika Tasnia hiyo huku Baadhi ya wasanii na wasambazaji
wengine kuanza kufuata mtindo wake wa Kupokea Filamu yenye Part 1 tu...
Proin Promotions inasema kwamba yenye hata kama story ikiwa na Masaa
kumi basi itakuwa katika DVD moja kuliko kumuibia Mtanzania ambae
anahitaji kupata kile anachostahili kwa bei nzuri huku akiwa haangaishwi
katika Kununua Story moja katika DVD mbili.
Mpaka
sasa tayari kuna baadhi ya Wasambazi na wasanii wameanza kufuata mtindo
huo wa kutoa Sehemu moja ya filamu tu huku wengine wakijitahidi kuweka
Dvd Mbili katika Kasha moja. Hili kwa Proin wanajivunia kutokana na watu
kuanza kuzoea mfumo wao walioingia nao Sokoni.
Na
Vilevile filamu za kitanzania nyingi zimeshaingia kwenye mfumo huo wa
part 1 na 2 huku baadhi ya wasanii au wasambazaji wakikataa kupokea
filamu yenye part 1 na 2.
Kampuni
ya Proin Promotions ni moja ya Kampuni ya Usambazaji, utengenezaji wa
filamu nchini ambayo iliingia sokoni na Staili ya kukataa Part 1 na 2,
huku filamu zake zote ni sehemu moja tu. Kampuni hiyo inayofanya vizuri
katika soko ikiwa na filamu ya MDUNDIKO ambayo ilichukua tuzo nchini
Marekani kutokana na ubora wa Story yake ambayo haikuwa na part 2,
Kampuni hii ya Proin Promotions ambayo mpaka sasa imeshatoa Filamu
takribani 16 na zote zikiwa zimefanya vizuri sokoni huku Filamu yake
Mpya iitwayo MAPENZI YA MUNGU ikiendelea kukimbiza Sokoni kwa kununuliwa
Kwa Wingi kutokana na Ubora wake na ni filamu ambayo imechezwa na Lulu,
Lina na Mama Kanumba. Proin Promotions ni Kampuni ambayo kwanza imeweza
kuleta mapinduzi katika Tasnia hii ya Filamu kwa kutonunua hatimiliki
ya Msanii wa filamu husika.
Hivi
karibuni Kampuni ya Proin Promotions Ltd itaingiza sokoni filamu yake
Mpya nyingine iitwayo NEVER GIVE UP iliyochezwa na Slim, Hashim Kambi,
Irene Paul na Staa wa Filamu Kutoka Nchini Ghana ajulikanaye kama VAN
VICKER. Filamu hii itakuwa sokoni kuanzia tarehe 10 November 2014 huku
ikiaminika kufanya vizuri zaidi sokoni.
Mpaka
Sasa Kampuni ya Proin Promotions imeshatoa Filamu kama, Foolish Age,
Long Time, Figo, Fedheha, Kitendawili, Siri Ya Mtungi Season 1 na Season
2, Kimbulu,Network, Sunshine, Mdundiko, I Love Mwanza, Joti Sanduku la
Babu, Family Curse, Nitadumu Nae, huku Mapenzi ya Mungu na Kigodoro
zikiwa ni filamu zinazofanya Vizuri mpaka sasa Sokoni.
Usikose nakala yako halisi ya Filamu moja wapo kati ya Hizo huku Ukiendelea kusubiri kwa hamu Filamu ya NEVER GIVE UP
No comments:
Post a Comment