Meneja mahusiano mwandamizi wa Benki ya Posta Tanzania (TPB) Noves Moses (kushoto)
 akimkabidhi jezi nahodha wa timu ya netiboli ya waandishi wa habari za 
michezo nchini (Taswa Queens) Imani Makongoro (Kulia) katika halfa fupi iliyofanyika makao makuu ya benki hiyo jana. Katikati ni Mwenyekiti wa Taswa SC, Majuto Omary . Picha/Mpigapicha wetu
*****************************************
Na Mwandishi Wetu, Dar
Benki ya Posta Tanzania (TPB) imeendelea kuisadia  timu ya   Waandishi wa habari za  michezo
 nchini (Taswa SC) baada ya kuikabidhi vifaa vya michezo kwa ajili ya 
kutumika katika mashindani na michezo mbali mbali ya kirafiki.
Benki
 hiyo imekabidhi seti za jezi kwa timu hizo zikiwa na jumla ya thamani 
ya Sh1,180,000 kwa timu ya mpira wa miguu maarufu kwa jina la Taswa FC 
na timu ya netiboli ambayo pia inajulikana kwa jina la Taswa Queens.
Akizungumza
 katika makabidhiano hayo, Meneja mahusiano mwandamizi wa Benki ya Posta
 Tanzania (TPB) Noves Moses alisema kuwa msaada huo ni sehemu ya 
shughuli za benki kijamii na kutambua mchango mkubwa wa waandidshi wa 
habari hapa nchini.
“Waandishi
 wa habari wameonyesha mfano mkubwa kwa kucheza soka na netiboli, pia 
niliona mnafanya mazoezi ya ngumi chini ya bondia Thomas Mashali, huu ni
 mfano wa kuigwa na ndiyo maana tumevutiwa na utendaji na maendeleo 
yenu,” alisema Noves.
Mwenyekiti
 wa Taswa SC, Majuto Omary aliishukuru TPB kwa kuendelea kuwakumbuka na 
kuahidi kutumia jezi hizo kwa kushinda mechi na wala si kutoka sare au 
kufungwa.
“Tunajivunia
 uwepo wa Benki ya Posta kwa kuthibitisha kuwa ni benki halisi ya 
Watanzania, nachukua fursa hii kuwaomba Watanzania kufungua akaunti zao 
katika benki hii na vile vile kuomba wadau wengine kufuata mfano wao kwa
 kuisaidia Taswa SC ili iweze kufanikisha ziara zake,” alisema Majuto.
No comments:
Post a Comment