WAKALA WA TAIFA WA HIFADHI YA CHAKULA (NFRA) KANDA YA DODOMA INAKABILIWA NA UFINYU WA ENEO LA KUHIFADHIA MAZAO MSIMU HUU WA UNUNUZI WA MAZAO
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi akikagua shughuli za ufungashaji mahindi na Mtama kwenye magunia tayari kwa kuhifadhiwa kwenye maghala wakati alipotembelea kituo cha NFRA Kanda ya Dodoma.
Wakinamama kwenye kituo cha Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Kanda ya Dodoma wakipeta mahindi na kuyaondoa uchafu tayari kwa ajili ya kuyafungasha kwenye magunia na kuyahifadhi ghalani, mahindi hayo yananunuliwa kutoka kwa wakulima na wafanyabiashara mbalimbali.
Moja ya maghala ya NFRA Kanda ya Dodoma ambayo yamejaa mahindi na Mtama na hivyo kuhitaji maeneo/maghala mengine zaidi ya kuhifadhia mazao.
Gari iliyobeba mahindi ikipima uzito ili kupeleka mahindi hayo kuhifadhiwa kwenye maghala kwenye kituo cha Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Kanda ya Dodoma, changamoto kubwa kituoni hapo ni uchache wa maghala ya kuhifadhia mazao hayo.
No comments:
Post a Comment