header

nmb

nmb

Thursday, May 8, 2014

WAREMBO MISS MBAGALA KUTAMBULISHWA 'DAR LIVE' KESHO



Kampuni ya PR Promotion inawaletea Kitongoji kipya katika mashindano ya Urembo Tanzania kupitia wilaya ya Temeke ambayo ni Miss Mbagala 2014.

 Warembo wote watatambulishwa rasmi siku ya ijumaa tarehe 9/5/2014 sambamba na uzinduzi rasmi wa Miss Mbagala 2014 katika ukumbi wa Dar Live kuanzia saa 2 usiku Mbagala jijini Dar es salaam.

Hii ni mara ya kwanza kitongoji cha Mbagala kuandaa mashindano ya Miss Tanzania baada ya kuongezwa na kamati ya Redds Miss Tanzania mwaka huu hivyo wilaya ya Temeke itakuwa na vitongoji vine ambavyo ni Changombe, Kurasini, Kigamboni na Mbagala.

Washindi watatu wa mwanzo watashiriki moja kwa moja katika mashindano ya Redds Miss Temeke 2014.

No comments:

Post a Comment