header

nmb

nmb

Tuesday, January 7, 2014


MAELFU   ya  wakazi  wa mkoa  wa Iringa na  baadhi  ya  viongozi  wa  vyama  vya  siasa na  Serikali  wakiongozwa na  Rais Dr  Jakaya  Kikwete  wameshiriki  katika mazishi ya  aliyekuwa  mbunge wa   jimbo la Kalenga na  waziri wa fedha  Dr  Wiliam Mgimwa.

Huku   waziri  mkuu Mizengo  pinda katika  salam  zake za serikali akielezea  jinsi ambavyo  Taifa  lilivyopata  pigo kubwa  kufuatia  kifo  cha Dr Mgimwa kutokana na mchango  wake  katika baraza la mawaziri.

Katika  mazishi  hayo   yaliyofanyika  leo kijiji  kwake Magunga  jimbo la Kalenga   wananchi   mbali  mbali   walionyesha  kujipanga  barabarani  kutoka Manispaa ya  Iringa  hadi  kijijini kwake  huku  wakiupungia mkono msafara  wa    rais Kikwete na baadhi yao  wakilazimika  kutumia  usafiri wa baiskeli na pikipiki  kwenda katika mazishi  hayo.

Akitoa   shukrani za  familia kwa niaba ya  familia  mtoto wa marehemu Dr Mgimwa Godfrey  Mgimwa  aliishukuru   serikali kwa  jinsi ambavyo ilivyohangaika  kumuuguza baba  yake  na  kutoa wosia  mzito wa marehemu  Dr Mgimwa ambao  alimtaka kuufikisha kwa Rais  Kikwete..

Alisema  katika  uhai  wake kabla  ya kifo  chake  ikiwa ni siku tano kabla  Dr  Mgimwa alimwita na  kumtaka  kufikisha  shukrani zake kwa Rais  Kikwete kwa  kumtembelea mara mbili Hospital  alipokuwa amelazwa  pamoja na  spika wa bunge Anne makinda .

Pia  alisema  kuwa alieleza dhamira  yake ya  kuwatumikia  wana Kalenga na  kusema  zawadi kubwa ni msaada wa bati  zaidi ya  2000 kwa wananchi hao  ili kuendeleza ujenzi wa shule na  vituo  vya afya  jimboni.

"Baba  kabla ya  kufa  aliniachia  wosia  huo juu ya wana Kalenga kwa kuwashukuru kwa  ushirikiano  wao na  kutoa  bati ila alipenda  kuona  Kalenga  inakuwa na maendeleo zaidi"

Kwa  upande  wake  waziri Mkuu Pinda  alisema  kuwa  serikali imepata pigo kubwa  juu ya kifo hicho na kuwa  bado serikali  itaendelea  kuwa karibu na familia ya Dr Mgimwa  na pale  penye tatizo  isisite  kuwasiliana .

Hata  hivyo  Rais  Kikwete  hakupata  kuzungumza  chochote  katika msiba  huo  zaidi ya  kuweka mchanga na shada la maua pamoja na kuwapa mkono  ndugu wa Dr Mgimwa .


Spika  wa bunge Anne Makinda  alisema kuwa  bunge  limempoteza kiongozi na mbunge aliyependa kutumia  nafasi yake kwa ajili ya Taifa  na kuwa kamwe mchango  wake  hawataacha kuukumbuka.
You might also like:

KONYAGI YAWAZAWADIA WAFANYAKAZI WAO WA MUDA MREFU

 Mkurugenzi wa Masoko wa Kiwanda cha Konyagi cha Tanzania Distilleries (TDL), Joseph Chibehe (kushoto) akimkabidhi cheti cha kwa kuwa mmoja wa wafanyakazi wa muda mrefu wa kampuni hiyo, Ashura Omari  wakati wa hafla ya wafanyakzi kufurahi pamoja na familia zao kwenye Hoteli ya Kunduchi Beach, Dar es Salaam. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa  TDL, David Mgwassa.
 Mkurugenzi Mtendajj wa Kiwanda cha Konyagi, David Mgwassa aimpatia Munisi cheti cha shukurani kwa kuwa mmoja wa wafanyakazi wa muda mrefu waliotumikia kiwanda hicho.

 Mgwassa akimtunuku Michael Mrema cheti kwa kuwa mmoja wa wafanyakazi wa muda mrefu wa TDL
 Wafanyakazi wa Kiwanda cha Konyagi na familia zao wakishindana kufukuza kuku
 Sssa ni wakati wa mapumziko
Watoto wa wafanyakazi wa TDL wakishindana mbio za magunia
You might also like:

No comments:

Post a Comment