Msichana huyo mwenye umri wa miaka 21 sasa hivi alisema Franck Ribery, mchezaji wa Bayern Munich alimtumia kama zawadi wakati wa sherehe za siku yake ya kuzaliwa mwaka 2009.
Inaripotiwa Ribery alimkatia msichana huyo tiketi ya ndege aweze kusafiri kutoka Ujerumani mpaka Ufaransa kumtumbuiza wakati wa kusherehekea siku yake ya kuzaliwa ambapo binti huyu anasema pia alilipwa ili afanye ngono na Karim Benzema wa Real Madrid.
Benzema amekanusha madai ya msichana huyu kwamba aliwahi kulipwa pia kufanya nae ngono hotelini huko Paris wakati binti akiwa na umri wa miaka 16.
Ribery amekubali kwamba kweli alifanya ngono na msichana huyu kama zawadi yake yabirthday lakini anasisitiza kwamba hakujua binti huyu hakuwa amefikisha umri wa miaka 18.
Hawa wakali wa soka wanaweza kufungwa jela miaka mitatu kila mmoja ikiwa watapatikana na hatia.
No comments:
Post a Comment