Afrika na dunia inatarajiwa kushuhudia
kitu kipya katika maziko ya Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson
Mandela (95) aliyefariki dunia juzi, baada ya kuugua kwa zaidi ya miezi
sita.
Serikali ya Afrika Kusini imesema
kiongozi huyo ambaye atazikwa Desemba 15, imeandaa mazishi ya kihistoria
yanayosemekana yatazidi yale ya Papa John 11.
Matukio ya shughuli mbalimbali
zinazohusu mipango ya maziko ya kiongozi huyo maarufu yanatarajiwa
kushuhudiwa sehemu mbalimbali duniani, tofauti na tukio jingine
lililowahi kutokea barani Afrika mbali na kombe la dunia.
Rais Jacob Zuma alisema jana kwamba
“Mpendwa wetu Madiba atazikwa kwa heshima zote za Serikali. Nimeagiza
bendera zote za Afrika Kusini zipepee nusu mlingoti na hiyo itaendelea
hivyo hadi tutakapokamilisha mazishi yake.
Mazishi ya Mandela yanalinganishwa na
yale ya Papa John Paul II mwaka 2005, ambayo yalihudhuriwa na wafalme
watano, malkia sita wa falme mbalimbali na marais wapatao 70 na mawaziri
kadhaa, wakiwamo wafuasi wake zaidi ya milioni mbili. Yanakadiriwa pia
kulingana na maziko ya Winston Churchil aliyekuwa Waziri Mkuu wa
Uingereza mwaka 1965.
Marais wote wa Marekani walio hai
wanatarajiwa kuhudhuria mazishi hayo iwapo afya zao zitawaruhusu
kusafiri, pamoja na Prince Charles wa Uingereza na hata Rais Robert
Mugabe wa Zimbabwe. Pia watu maarufu wenye urafiki wa karibu na Mandela
akiwamo msanii Oprah Winfrey wameshathibitisha kuhudhuria.
No comments:
Post a Comment