Msemaji toka Wizara ya Kazi na Ajira Bw.Ridhiwan Wema(Kulia) akieleza kwa waandishi wa habari kuhusu majukumu ya Bodi za
Mishahara Kisekta kwa mujibu wa sheria Na. 7 ya Mwaka 2004 ya Taasisi
za Kazi katika Sekta Binafsi, wakati wa Mkutano uliofanyika katika
ukumbi wa Idara ya Habari(MAELEZO) Leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni
Mchumi Mwandamizi wa Wizara hiyo Bw. Jofrey Mashafi.
*************************************************
Moja ya majukumu ya Wizara ni kusimamia utekelezaji wa Sera na Sheria za Kazi mahali pa Kazi.
Bodi za mishahara kisekta zinaundwa kwa mujibu wa sheria ya Taasisi za Kazi Na 7 ya mwaka 2004.
Sheria hii inampa mamlaka Mh.Waziri wa Kazi na Ajira kuunda bodi hizo kwa kuteua wenyeviti na wajumbe wa bodi hizo.
Mwakak 2007 kwa kuanzia Mhe.Waziri wa Kazi aliunda bodi 8 za mishahara kwa sekta binafsi.
Bodi hizo ni katika sekta zifuatazo:-
(i)
Kilimo (ii) Afya (iii) Biashara na
viwanda (iv) Mawasiliano (v) Madini (vi) Uvuvi na huduma za
majini(vii)Hoteli na huduma za majumbani (viii)Ulinzi binafsi.
Mwaka 2011 ziliongezeka bodi mpya 4 ambazo ni(i)Usafirishaji (ii) Shule binafsi (iii) Ujenzi (iv) Nishati
Hivyo hadi sasa mwaka 2013 idadi ya bodi zilizopo ni 12.
Muundo wa Bodi
Kila
Bodi inaundwa na wajumbe 8 akiwemo Mwenyekiti na wajumbe wanaowakilisha
maslahi ya Serikali Wajumbe 2,Waajiri Wajumbe 2 na Wafanyakazi 2 katika
mfumo wa Utatu (TRIPATISM), pamoja na wajumbe wengine wanaoteuliwa kwa
kuzingatia utaalamu wao katika masuala ya Kazi na Ajira, Mtaalam huyu
anakuwa mmoja.
MAJUKUMU YA BODI.
Majukumu ya Bodi yameaninshwa chini ya kifungu cha 36 (1) cha sheria ya Taasisi za Kazi Na 7 ya mwaka 2004 ambayo ni pamoja na:-
(a) Kufanya uchunguzi kuhusu kima cha chini cha mishahara na hali ya Ajira katika sekta husika.
(b) Kuandaa
na kuwasilisha mapendekezo kwa Mhe.Waziri wa Kazi kuhusu kima cha chini
cha mshahara pamoja na masharti ya Ajira katika sekta husika
(c) Kuhamasisha majadiliano ya pamoja (collective bargaining) sehemu za Kazi kati ya vyama vya wafanyakazi na waajiri.
Kifungu
cha 42 (2) cha sheria hii, kinaruhusu Mtaalamu mwelekezi apewe
kandarasi katika kutekeleza majukumu ya Bodi ikiwemo suala la kufanya
utafiti (a) wa Kima cha chini cha Mishahara.(a) Pamoja na yaliyoelezwa hapo juu,Baraza la Kazi,uchumi na Jamii (LESCO) litapitia
mapendekezo ya Bodi za Mishahara na kutoa maoni na ushauri kwa
Mhe.Waziri wa Kazi,ambaye ndio mwenye mamlaka ya kutangaza vima vya
chini vya mishahara kwa kuzingatia ushauri uliotolewa.
Viwango vya Mishahara:
Viwango
vinapaswa kuzingatia maoni ya pande zote za wadau pamoja na ushauri wa
vyombo vingine vyenye mamlaka chini ya sheria ,kwa kuzingatia
yafuatayo:-
(i) Uwezo wa waajiri kufanya biashara /shughuli kwa ufanisi.
(ii) Uanzishaji na uendeshaji wa biashara /shughuli ndogo na za kati.
(iii) Gharama za maisha
(iv) Uanzishwaji wa biashara mpya.
(v) Kuondoa umaskini
(vi) Kiwango cha chini cha kujikimu (i) Mishahara na hali za Ajira za Wafanyakazi walioajiriwa katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kwenye sekta husika
(ii) Madhara
yanayoweza kujitokeza katika Ajira iliyopo na kuanzishwa kwa ajira mpya
kutokana na mapendekezo yatakayotolewa.
UPANGAJI WA KIMA CHA CHINI CHA MISHAHARA KISEKTA KUPITIA TANGAZO LA MISHAHARA NA.196 LA MWAKA 2013 NA UTARATIBU ULIOFUATWA.
Kima
cha chini cha mishahara katika sekta binafsi 12 kilitangazwa
tarehe 28/6/2013 kupitia Tangazo la Serikali Na.196, mishahara mipya
ilianza kutumika rasmi tarehe 1 Julai 2013.
Taratibu zilizofanyika:-
(1) Bodi
za mishahara kisekta zilitembelea maeneo mbalimbali ya kazi nchini
katika mikoa 11, ambayo
ni:-
Dar es salaam, Morogoro,Pwani,Dodoma,Arusha,Mwanza,Tanga,Manyara,Iringa,Mbeya na Kilimanjaro.
Lengo
likiwa ni kujionea hali halisi ya mazingira ya kazi na kupata maoni ya
wadau kuhusu kima cha chini cha mishahara katika sekta husika.
(1) Mtaalam
mwelekezi ambaye alikuwa Chuo cha Utumishi wa Umma alitembelea
mikoa 20 kwa ajili ya utafiti na matokeo ya utafiti yalitumiwa na
bodi 12 katika kuandaa mapendekezo ya mishahara.
(2) Katika utafiti uliofanywa Mtaalamu mwelekezi alionana na Waajiri zaidi ya 398 na Wafanyakazi zaidi ya 1329.
Aidha wadau pia walipewa fursa ya kutoa maoni yao kupitia magazeti ya Mwananchi na Daily News ya tarehe 11/02/2103
USHAURI NA MAPENDEKEZO
(I) Tangazo
la Serikali Na.196 la mwaka 2013 linaelekeza kiwango cha kuanzia au
kima cha chini cha mshahara.Waajiri wanayo nafasi ya kuboresha kima
hicho kutegemeana na Tija na uwezo wa kampuni kulipa, kima hiki ni
Elekezi.
(II) Vyama
vya Wafanyakazi vina nafasi kubwa kuboresha mishahara na maslahi ya
Wafanyakazi kupitia majadiliano ya pamoja (collective barganing) sehemu
za Kazi, kwa kuwa sheria na kanuni zinatoa na kuhimiza haki hiyo.
(III) Makampuni ya ujenzi yanayolalamika kuingia M
(IV) ikataba isiyobadilika
katika kandarasi za ujenzi, tunayashauri kuwasiliana na Wateja wao ili
kurekebisha mikataba yao kwa lengo la kukidhi mahitaji ya kima cha chini
cha mishahara kama inavyofanyika kwa vitendea kazi wanavyovitumia pale
vinapopanda bei.
IMETOLEWA
RIDHIWANI M.WEMA
Msemaji
WIZARA YA KAZI NA AJIRA.
No comments:
Post a Comment