Meza Kuu ya viongozi katika hafla hiyo.
Makamu
wa Rais, Dkt. Mhammed Gharib Bilal, aliyekuwa mgeni rasmi katika Hafla
ya Chakula cha Hisani iliyoandaliwa na AMREF Tanzania kwa kushirikiana
na Montage Limited na Benki M, maalum kwa ajili ya kuchangisha fedha kwa
Kampeni ya Simama kwa ajili ya akinamama wa Afrika, akipokea mfano wa
hundi yenye thamani ya Sh. Milioni 25, kutoka Kwa Mwakilishi wa Benki ya
NBC, wakati wa hafla hiyo iliyofanyika jana usiku kwenye Hoteli ya
Serena jijini Dar es Salaam. Kampeni hiyo ina lengo la kukusanya fedha
kwa ajili ya Kusomesha Kinamama wakunga ili kusaidia kupunguza Vifo vya
Mama na Mtoto, ambapo jumla ya Sh. milioni 719 zilipatikana wakati wa
hafla hiyo. Kulia ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Hussein
Mwinyi.
Miongoni mwa wadau waliofanikisha mkutano huo walitunukiwa vyeti vya kutambua mchango wao.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akihutubia wakati alipokuwa mgeni rasmi katika hafla ya Chakula cha
Hisani ya kuchangisha fedha kwa ajili ya Kampeni ya Simama kwa ajili ya
akinamama wa Afrika, iliyofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es
Salaam jana usiku. Katika hafla hiyo jumla ya Sh. milioni 719,
zilipatikana. KUSOMA ZAIDI BOFYA READ MORE
*MARAFIKI WA MEMBE PAMOJA NA WANAFUNZI WA CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWL NYERERE WATEMBELEA HOSPITALI YA KIGAMBONI NA KUFANYA USAFI
Baadhi
ya wanafunzi wa Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwl Nyerere kilichopo Kigamboni
Jijini Dar wakifanya usafi katika mazingira ya Hospitali ya Kigamboni
wakati walipoenda kutembelea hospitali hiyo kwaajili ya Kufanya usafi na
kuwafariji wagonjwa ikiwa wanaadhimisha siku ya Mwl Nyerere Chuo hapo
Baadhi
ya wadau waliohudhuria katika kufanya usafi na kuwatembelea wagonjwa
katika hospitali ya Kigamboni hapo jana wakati wanafunzi wa Chuo Cha
Kumbukumbu ya Mwl Nyerere Kwa kushirikiana na Marafiki wa Membe
Wakiongozwa na Kijana Allan walipotembelea hospitali hiyo ikiwa
wanaadhimisha Siku ya Mwl Nyerere
Baadhi ya wanafunzi na wadau waliojitolea kwenda kutembelea hospitali ya Kigamboni hapo jana
Mmoja
wa Wanafunzi wa Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwl Nyerere akitoa msaada wa
Mche wa Sabuni kwa Mmoja wa wagonjwa waliokuwa wamelazwa katika wodi ya
wazazi iliyopo katika hospitali ya Kigamboni wakati wanafunzi wa chuo
hiko pamoja na Marafiki wa Membe walipoenda kutembelea Hospitali hiyo
kwa kufanya usafi na kuwafariji wagonjwa ikiwa wanaadhimisha siku ya Mwl
Nyerere
Baadhi
ya wanafunzi na Wadau wa Marafiki wa Mh Membe wakiwa wamebeba Mabango
yenye ujumbe wakati walipotembelea hospitali ya Kigamboni Kwaajili ya
Kufanya Usafi na kuwafariji wagonjwa hapo jana.Picha na Josephat Lukaza
No comments:
Post a Comment