Mkurugenzi Mkuu wa TDL akiwa na Mabosi wa SABMILLER
AFRICA.wakiwa wameshikilia tuzo hiyo ya MB COMPLEMENTARY BEVERAGE CATEGORY
AWARD FOR (F 13)
PICHA NDOGO CHINI NI BAADHI YA WAFANYAKAZI TDL WALIO TEULIWA KWENDA KUTIZAMA KABUMBU UGHAIBUNI
PICHA NDOGO CHINI NI BAADHI YA WAFANYAKAZI TDL WALIO TEULIWA KWENDA KUTIZAMA KABUMBU UGHAIBUNI
CHIBEHE MZEE WA TANZANIA
KAMPUNI ya Tanzania
Distilleries Ltd (KONYAGI) imeshinda tuzo ya utendaji bora wa bidhaa (SABMILLER
AFRICA MB COMPLEMENTARY BEVERAGE CATEGORY
AWARD FOR F 13), ni miongoni mwa Kampuni tanzu za Sabmiller ya Afrika Kusini.
Akiongea na waandishi
wa Habari, Dar es Salaam leo, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Konyagi ya Tanzania Distilleries Limited
(TDL), David Mgwassa, aliyepambana mpaka kupatikana kwa ushindi huo. amesema kuwa wanajivunia kuwa
washindi miongoni mwa makampuni mengi yaliyo chini ya Sabmiller.
“Ushindi huu ni
ishara kubwa ya mafanikio KONYAGI na sisi hatutarudi nyuma hii ni chachu katika
kutufanya tuendelee kuzalisha bidhaa bora na zenye viwango vya hali ya juu kwa
bei nafuu na kuzishinda kampuni zingine” alisema Mgwassa.
Amesema kuwa
ushindani ulikuwa mkubwa sana mana kila Kampuni
miongoni mwetu inajitahidi kuzalisha bidhaa kwa kiwango cha hali ya juu na sisi
kushinda ni ishara kuwa bidhaa zetu zinakubalika kila mahali hapa Africa hata
nje ya Africa.
Licha ya kupewa tuzo
ya ubora, pia TDL imepewa nafasi kwa Wafanyakazi wake watano kwenda kuangalia mpambano mkubwa la ligi kuu ya
Hispania (LA LIGA) kati ya Barcelona na Real Madrid.
Mgwassa
aliwataja
wafanyakazi wanaokwenda Hispania kuangalia mechi hiyo kuwa ni Joseph
Chibehe, Khadja Madawili, Bavon Ndumbati, Michael Mrema na Mwesige
Mchuruza.
No comments:
Post a Comment