header

nmb

nmb

Friday, October 25, 2013

KONYAGI YASHINDA UBORA WA BIDHAA, YAPAA KWENDA HISPANIA KUCHEKIKABUMBU


Mkurugenzi mkuu wa TDL akiwa naMabosi wa (SABMILLER AFRICA.Wakiwawameshikiliatuzo hiyo ya  MB COMPLEMENTARY BEVERAGE CATEGORY AWARD FOR (F 13)


PICHA NDOGO CHINI NI BAADHI YA WAFANYAKAZIWALIO TEULIWA KWENDA KUTIZAMAKABUMBU MBELEHUKO
                                                            MWEISIGA MZEE WA JIJI
                                                 CHIBEHE MZEE WA TANZANIA
                                                    BI, KHADIJA MKUU WA MSAFARA
                                       HUYU NDIOMREMAMZEE WA MWANZA

 Mkurugenzi Mkuu wa kamuni ya TDL David Mgwassa aliepambana mpaka kupatikana kwa ushindi huo.
KAMPUNI ya Tanzania Distilleries Ltd (KONYAGI) imeshinda tuzo ya utendaji bora wa bidhaa (SABMILLER AFRICA MB COMPLEMENTARY BEVERAGE CATEGORY AWARD FOR F 13) miongoni mwa Kampuni tanzu za Sabmiller ya Afrika Kusini.

Akiongea na waandishi wa Habari Mkurugenzi Mkuu wa TDL David Mgwassa, amesema kuwa wanajivunia kuwa washindi miongoni mwa Makampuni mengi yaliyo chini ya Sabmiller.

“Ushindi huu ni ishara kubwa ya mafanikio KONYAGI na sisi hatutarudi nyuma hii ni chachu katika kutufanya tuendelee kuzalisha bidhaa bora na zenye viwango vya hali ya juu kwa bei nafuu nakuzishinda kampuni zingine” alisema Mgwassa.

Amesema kuwa ushindani ulikuwa mkubwa sana mana kila Kampuni miongoni mwetu inajitahidi kuzalisha bidhaa kwa kiwango cha hali ya juu na sisi kushinda ni ishara kuwa bidhaa zetu zinakubalika kila mahali hapa Africa hata nje ya Africa.

                                                            ZAWADI YA KWENDA

Licha ya kupewa tuzo ya ubora, pia TDL imepewa nafasi kwa Wafanyakazi wake watano wamepewa nafasi ya kuangalia mpambano mkubwa la ligi kuu  ya Hispania (LA LIGA) kati ya Barcelona na Real Madrid.
habari zaidi zinakuja baada ya muda mfupi

Mgwassa aliwataja wafanyakazi wanaokwenda Hispania kuangalia mechi hiyo kuwa ni Joseph Chibehe, Khadja Madawili, Bavon Ndumbati, Michael Mrema na Mwesige Mchuruza.

No comments:

Post a Comment