Kituo cha Amani na
utafiti wa migogoro Africa kilianzishwa mwaka 2012 na wataalamu wa Masuala ya
Amani ya Kimataifa na utafiti wa migogoro ambao ni wahadhiri wa vyuo vikuu.
Wahadhri hao pamoja na wanafunzi wa fani hii ya amani wameguswa na jinsi
ambavyo Bara la Africa limekumbwa na kugawanywa na migogoro ya kivita.
Wataalamu hawa wana lenga kumaliza migogoro hii kwa njia ya utafiti wa kina,
kukusanya takwimu na kuchapisha ikiwa ni pamoja na kutoa mafunzo,na kusuluhisha
migogoro.
Kituo hiki
kikiongozwa na tunu kubwa ya Haki na
Amani ni chombo ambacho kina lenga kujenga amani ya kudumu Africa Mashariki,
Africa ya Kati na Africa kwa ujumla tukianzia na Tanzania. Kituo hiki
kimeanzishwa kushughulikia amani ambayo katika bara la Africa imekuwa kitu
adimu. Kituo cha amani na migogoro ni namna nyingine ya kuzungumza na kujadili
amani.
Kwa nini Tanzania
kuwa na kituo kama hiki?
Tanzania ni mmoja
katika nchi chache barani Africa sio tu kuwa ilipata uhuru wake kwa njia ya
amani bila umwagaji wa wazi wa damu lakini pia ni mmoja kati ya nchi chache
ambayo hajaingia katika utawala wa kidicteta, au wa kijeshi au kuwa na vita
rasmi. Hii ni bahati kwa kuwa kuna baadhi ya nchi barani Africa ambazo tangu uhuru
katika miaka ya sitini hazijawahi kuwa katika hali kama hiyo. Hata hivyo pamoja
na upande huu mzuri, hapa Tanzania tumeanza kushuhudia viashiria ambavyo iwapo
havitafanyiwa kazi mapema na kwa utaratibu wa kitaalamu tunaweza kujikuta
katika hali ambayo nchi nyingi barani Africa zimejikuta. Hii inatokana na
ukweli kuwa Amani ni tunu na kama ni tunu ni lazima itunzwe na ilindwe siyo kwa
bunduki au kwa vurugu bali kwa haki na utulivu. Kuna viashiria vya wazi ambavyo
vinaweza kuwa sumu ya kuvuruga amani ya nchi yetu.
Kwanza, ushindani wa
kisiasa: Kuna kila dalili kuwa ushindani wa kisiasa unataka kufanyika kwa
kutumia nguvu. Hii tunashuhudia pale tunapoona mikutano ya hadhara
ikishambuliwa, kukitokea vurugu wakati wa mikutano ya kisiasa, hadi watu
kupoteza maisha yao. Upinzani unavyozidi kuwa na nguvu vurugu nazo zinaonekana
waziwazi.
Pili, ni suala la
maliasili kama vile madini, ardhi, nishati za aina zote n.k. Barani Africa hiki
ni chanzo kikuu cha vita. Hapa nchini tunashuhudia wananchi wakipambana na wawekezaji,
wananchi wakipambana na serikali, kuna hali ya sintofahamu.
Tatu, wakulima na
wafugaji. Ugomvi wa wakulima na wafugaji sio tu ule wa kimila wa zamani lakini
sasa unaenda katika hatua ya juu zaidi ambapo kumekuwa na matokeo mabaya ya
ugomvi huo.
Nne, ni suala la
dini, ambalo hivi sasa linachukua sura nyingi. Kuanzia kujeruhiwa, hadi kuuuwa
kwa wale ambao tunaweza kusema ni viongozi wa dini.
Haya matatizo tunayo
hapa nchini na ukubwa wake na hatari yake kutoshughulikiwa kitaalamu
inawezekana yasionekana leo lakini miaka michache ijayo tunaweza kuingia katika
mgogoro ambao kuutatua itakuwa ni kazi
ngumu zaidi kuliko kuchukua hatua sasa
na kuzuia.
Hivyo basi Kituo cha
amani na utafiti wa migogoro kinachukua hatua zifuatazo katika mipango yake:
1Elimu ya Amani (
Peace Education)
1.
.Utafiti, uandishi na uchapishaji
2.
Mafunzo mbalimbali kuhusu amani
3.
Mazungumzo, usuluhishi na ujengaji wa amani
Maeneo haya
yatatekelezwa kwa njia zifuatatzo
a) Mafunzo na elimu
b) Semina na warsha
c) Ufuatiliaji na uhamashishaji
d) Kujenga uwezo
e) Kuvishirikisha vyombo vya habari katika kujenga amani
Tumesema kuwa ili
kuzuia yale yanayoonekana hivi sasa hapa nchini kama hatari ya amani
tunahitaji kutumia mbinu za kitaalamu
ambazo ni pamoja na elimu kwa umma lakini i pia kukazia kuwepo kwa sera za
amani katika taasisi kama vile za elimu. Katika kuhamashisha amani tayari kituo
cha amani na utafiti wa migogoro Africa kinashirikiana na Kituo cha Sheria na
Haki za binadamu katika kutoa vipindi vya Radio na Televiisheni. Aidha tupo
katika mazungumzo na Tume ya Taifa ya UNESCO kuhusu utoaji wa elimu ya amani katika
taasisi na sekta za elimu. Ushirikiano huo upo katika hatua ya mazungumzo
ambapo serikali itakuwa na nafasi yake. Pia katika mgogoro wa Mtwara kituo hiki
kimetoa ushauri mbalimbali kuhusu mgogoro wa Mtwara.
Pia tumekuwa
tikivishawishi vyuo vikuu hapa nchini kutoa elimu hii ya Amani katika ngazi
mbalimbali. Tumeweza kutoa ushawishi huu kwa chuo kikuu cha Bagamoyo ambapo
kuanzia mwezi wa kumi watakuwa na degrii ya udhamili ya “Peace Studies and
Conflict Resolution”. Tunawahamashisha waandishi wa habari kuchukua kozi hii
kwani itawapa mwanga mkubwa katika kutoa habari za migogoro mbalimbali. Vyuo
vikuu vingine vipo vinajipanga katika kuanzisha kozi hii. Na haya ni matunda ya
Kituo cha Amani na utafiti wa Migogoro Africa.
Sio tu tunalenga
taasisi za elimu lakini pia tasnia nyingine kama za wasanii na wengineyo. Hivyo
basi tuko mbioni kuanzisha tuzo mbalimbali za amani.
Kituo cha amani na
utafiti wa migogoro Africa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali tutakuwa na
tuzo ya amani kama ifuatavyo:
A) Tuzo ya mwandishi wa
habari bora na chombo cha habari bora kwa kuhamasisha
amani,tukijua kuwa vyombo vya habari ni wadau wakuu wa amani.
B) Tuzo ya msanii bora
wa muzuki ambaye atakuwa na wimbo wenye maudhui ya amani na kukubalika katika jamii
C) Tuzo ya mwanafunzi
bora ambaye ataandika insha
inayohamasisha amani katika jamii.
Utaratibu wa kushiriki katika tuzo hizi
utatangazwa hapo baadaye. Tuzo hizi zitakuwa zikitolewa kila mwaka wakati wa
Maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Amani Duniani ambayo huadhimishwa kila mwaka tarehe 21 septemba. Kituo
cha amani na utatuzi wa migogoro kiko tayari kushirikiana na wadau wote wa
amani ili kuhakikisha kuwa lugha ya mtanzania inakuwa siyo migogoro bali AMANI.
Kituo cha Amani na Utafiti wa Migogoro
Afrika kina watakia AMANI katika kazi zenu.
Mtendaji Mkuu
Lioba Mpore.
No comments:
Post a Comment