Askari hao waliokufa ambao walikuwa
kwenye vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa huko nchini Sudan
ni Sajenti Shaibu Othuman, Koplo Oswald Chaula, Koplo Mohamed Juma,
Koplo Mohamed Chikilizo, Pte. Rodney Ndunguru, Pte. Peter Werema na Pte.
Fortunatus Msofe.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana
kwenye mtandao ni kwamba askari hao walikwenda kujaribu kumwokoa mwenzao
(ambaye hakutajwa) ambaye alisemekana kutekwa na vikosi vya waasi
nchini humo.
Wakati wakijiandaa, ghafla walizingirwa na askari hao waasi na kisha kushambuliwa kwa risasi hadi kufa.
Haikufahamika hali ya askari huyo ambaye alidaiwa kutekwa kama bado yu hai ama ni miongoni mwa waliokufa.
Mungu azilaze roho za askari wetu mahali pema peponi, Amina.
No comments:
Post a Comment