Huku rais mstaafu wa Afrika Kusini Nelson Mandela akiendelea kuugua
mjini Pretoria, jamaa zake wamejikuta kwenye malumbano kuhusu mgogoro
ambao umejitokeza wazi kwenye vyombo vya habari.
Badhi ya jamaa za familia wamemshtaki mjukuu mkubwa wa Mandela, Mandla,
katika juhudi za kutaka kufukua maiti za wanawe watatu wa Mandela ili
wawazike katika makaburi ya Qunu, ambako Mandela anataka azikwe.
Na Mgogoro kuhusu kutaka kuwafukua wafu hao ni ishara ya mgawanyiko
mkubwa katika familia kubwa ya Mandela, wake zake watatu , watoto sita
na wajukuu 17 na vitukuu
12 . Kulingana na baadhi ya viongozi wa
kijamii, wakati familia yake inapoendelea kuzozana , roho ya Mandela
haiwezi kuwa na aman
amaa kumi na sita wa familia ya Mandela pamoja na viongozi wa kijamii
wiki jana walipewa idhini ya muda na mahakama kufukua maiti hao na
kuwapeleka katika mji wa
Qunu, ambako makaazi ya Mandela yapo.
Lakini Mandla Mandela, ambaye kulingana na
vyombo vya habari, alihamisha maiti hao umbali wa kilomita 22 kutoka mji
wa wa Qunu hadi nyumbani kwake eneo la Mvezo mnamo mwaka 2011, anapinga
uamuzi huo.
Watatu hao walifukuliwa bila ya idhini ya familia yote ya Mandela na
viongozi wa kijamii wa ukoo wa AbaThembu ambao pia ni ukoo wa Mandela.
Wanaamini kuwa roho ya Mandela, ina sumbuka hivi sasa kutokana na mzozo kwenye familia yake na ndio maana roho yake haikatiki.
No comments:
Post a Comment