header

nmb

nmb

Monday, May 20, 2013

wananchi jijini Dar es Salaam wafurahishwa na uamuzi wa kuondolewa kwa hoja ya kupiga marufuku viroba



Joseph Chibehe
National Sales Manager
Tanzania Distilleries Ltd
(+255 764 703 027 Ê  È+255 767 266 601 P.O Box 9412 | Dar es Salaam | Tanzania, United Republic of
joseph.chibehe@tz.sabmiller.com
 

Baadhi ya wananchi jijini Dar es Salaam,
  wamepongeza hatua ya kundolewa bungeni kwa hoja

ya kupiga marufuku biashara ya Vinywaji vikali maarufu kama Viroba.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, katika maeneo

mbalimbali ya starehe jijini Dar es Salaam jana,

walisema hatua hiyo imewafurahisha kwani

imewafanya sasa kuachana na uamuzi wa kurudia

kunywa tena pombe haramu ya gongo ambayo ni

hatari kwa afya zao.

Akielezea furaha yake, Adamu Mwaituka ambaye

alikutwa katika Baa ya Way Point eneo la Banana,

Ukonga, Dar es Salaam, alisema uamuzi huo

ameupokea kwa chereko kwani hicho  kinywaji

 anakipenda na kukitumia mara kwa mara.

Kwa upande wa mnywaji Fikiri Abdallah,ambaye

alikutwa akimimina viroba kwenye glasi katika Baa ya

Mama Seles, Banana, Ukonga, yeye  alisema kuwa uamuzi

huo wa bunge kuacha kupiga marufuku viroba,

umemuokoa yeye na wenzie ambao afya zao

zilidorora walipokuwa wakinywa pombe haramu ya

gongo, lakini tangu waanze kunywa viroba miili yao

ina afya njema.

Akielezea athari mbazo zingetokea endapo, kinywaji

hicho kingepigwa marufuku, Suzan Amandus, mkazi

wa Ilala Mchikichini, alisema kuwa wengi wa watu

wenye kipato duni, wangenyimwa haki ya kutumia

kinywaji hicho na kurudia  tena kunywa pombe

haramu zinazotengenezwa kienyeji.


Meneja wa Baa ya New Somba Park, iliyopo

Mwembeyanga, Temeke, Idrisa Chande, alisema

alifurahi sana baada ya kusikia hoja ya kupiga

marufuku viroba imesimamishwa, kwani wangefanya hivyo biashara

ingeyumba kwa vile wateja wake wengi ni watumiaji  wa kinywaji hicho.

Hivi Karibuni ulizuka mjadala Bungeni, ambapo

baadhi ya wabunge wachache walitoa hoja wakati wa

kikao cha makadirio ya bajeti ya Wizara ya Afya na

Ustawi wa Jamii, kuwa kinywaji aina ya kiroba kipigwe

marufuku wakidai kwamba aslimia kubwa ya

madereva hunywa na kusababisha ajali.

Akihitimisha hoja ya makadilio ya bajeti ya wizara

hiyo, Waziri wa Afya na Ustawi, Dk. Hussein Ali

Mwinyi, alisema kuwa hawawezi kutoa uamuzi juu ya

suala hilo mpaka watakapojadiliana kwa pamoja kati

ya wizara husika na wazalishaji wa vinywaji hivyo.


No comments:

Post a Comment