Charles Gabriel ‘Chaz Baba,’ akimvisha pete mchumba’ke, Rehema Sospeter.
Tukio hilo lililoshuhudiwa na Amani lilijiri Mei 11, mwaka huu ndani ya
Ukumbi wa Business Park, Kijitonyama, Dar, wakati bendi yake ilipokuwa
ikitambulisha albam mpya, Risasi Kidole.
Akizungumza na paparazi wetu
mapema wiki hii, Chaz Baba alisema ameamua kuonesha uamuzi wake huo
kuanzia kwa mashabiki wake waliofika ukumbini na kwa wale wasiofika kwa
sababu wengi wao walikuwa hawamuamini.
“Nilifanya vile kukata
vilimilimi ‘coz’ tangu nimegawa kadi za mchango wa harusi, kumekuwa na
maswali mengi ambayo yanaashiria wengi hawaamini uamuzi wangu,” alisema
Chaz.
No comments:
Post a Comment