header

nmb

nmb

Friday, May 10, 2013

Binti (albino) Asimamishwa shule kwa Tuhuma za Ushirikina

Amina Mwamkinga alisema tangu tarehe tisa amefukuzwa bwenini na wanafunzi wenzie wakitaka aondoke shuleni hapo wakimtuhumu kuwa mchawi majira ya usiku hali iliyomlazimu kuomba hifadhi kwa mlinzi aliyemkubalia na kukesha naye hadi asubuhi  hali iliyopelekea kupigwa na baridi kali kutokana na kukosa nguo za kujisitiri kama Shuka nk.
Hapa Amina akimsimulia mkasa mzima mwandishi wa Mbeya yetu Joseph Mwaisango mara baada ya kupata maelezo yote ya Amina mwandishi wetu alimpigia simu katibu wa chama cha maalbino mkoa wa Mbeya afike ofisi ya Mbeya yetu ili wasaidiane kutatua tatizo hilo
katibu wa Chama cha Albino Mkoa wa Mbeya, Wiliamu Simwale alifika ofisi ya Mbeya yetu na kuanza kumsikiliza Amina katika ofisi ya Mbeya Yetu

No comments:

Post a Comment