RC Rukwa Mhadinsi Stella Manyanya
............................................................................................
Na Elizabeth Ntambala FG Blogu ,Sumbawanga
WATOTO wawili wamekufa maji katika matukio mawaili tofauti kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha mkoani Rukwa.
Katika tukio la kwanza lililotokea April 19 majira ya saa 5;46 asubuhi Joseph Lucas (6) mkazi wa Majumbasita mjini Sumbawanga alikufa maji baada ya kutumbukia kwenye dimbwi la maji akiwa anacheza na wenzake.
Baada ya mtoto huyo kutumbukia kwenye dimbwi alilia kuomba msaada lakini wenzake aliokuwa akicheza nao walishindwa kutoa msaada kutokana na umri wao kuwa mdogo hali iliyosababisha kufa.
Katika tukio jingine Anastela Kantalamba (12) mkazi wa kijiji cha Chipu nje kidogo ya Manispaa ya Sumbawanga alikufa maji baada ya kuzama kwenye dimbwi la maji machafu.
Kamanda wa polisi mkoa wa Rukwa Jacob Mwalwanda alisema kuwa tukio hilo lilitokea April 19 majira ya saa 6;30 mchana mara baada ya mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali kukatika.
Aidha baada ya mvua hiyo watoto walianza kuchezea maji machafu yaliyokuwa kwenye dimbwi na kuingia ndani zaidi hali iliyosababisha kunywa maji mengi na kufariki dunia.
Kamanda huyo alisema kuwa katika tukio jngine polisi mkoani humo linamshikilia Samora Mateo (33) mkazi wa Namanyere wilayani Nkasi baada ya kumkamata akiwa na nyara za serikali.
Alisema kuwa baada ya polisi kupata taarifa za siri walimsubiri njiani mtuhumiwa alifika akiwa anaendesha pikipiki aina ya Sanya yenye namba za usajili T242BQV akiwa amebeba mfuko wa salfeti na ndani yake kukiwa na meno mawili ya tembo yenye thamani ya shilingi 11,250,000.
Kamanda Mlwanda alisema kuwa mtuhumiwa huyo anahojiwa na mara baada ya upelelezi huo atafikishwa mahakamani ili kujibu tuhuma zinazo mkabiri.
Mwisho.

No comments:
Post a Comment