Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Eng. Ngosi Mwihava akifungua
Kikao cha wadau kuhusu kanuni za matumizi salama ya Bioteknolojia ya
kisasa, kikao kilihusisha wanasanyansi, wanasheria, Mtandao wa wakilishi
wa wakulima na Taasisi za Mbegu.
Wadau wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Katibu Mkuu Eng. Ngosi
Mwihava mara baada ya ufunguzi wa Kikao kazi cha wadau kuhusu kanuni za
matumizi salama ya Baiotoknolojia ya kisasa kikao kilichofanyika kwenye
Ukumbi wa Mikutano Ofisi ya Makamuwa Rais Mtaa wa Luthuli JijiniDar es
Salaam.{Picha na Ali Meja]
Naibu Katibu Mkuu Eng. Ngosi Mwihava (Kulia) akibadilishana mawazo na
Dr. Alois Kullaya kutoka Kituo cha Utafiti cha Mikocheni mara baada ya
kufungua kikao cha kanuni za Matumizi salama ya Baiotoknolojia ya
kisasa[Picha na Ali Meja]
Baadhi ya Wadau wakifuatilia mjadala, katika kikao kazi
kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Makamu wa Rais,
Mtaa wa Luthuli jijini Dar es Salaam leo.
Na Lulu Mussa
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Eng. Ngosi Mwihava
amewataka wadau kutoka sekta mbalimbali kujadili na kutoa maoni kuhusu
utekelezaji wa kanuni za matumizi salama ya Bioteknolojia ya kisasa ambazo ni
sehemu ya utekelezaji wa Sheria ya Mazingira na utekelezaji wa Itifaki ya
Cartagena chini ya Mkataba wa Hifadhi Bioanuai.
Akifungua kikao kazi, Eng. Mwihava amesema, Tanzania iliridhia
Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Bioanuai mwezi machi , 1996 na
kufuatiwa na Mkutano wa wanachama
ulioazimia kuandaa itifaki kuhusu
usalama wa Mazingira dhidi ya Athari za Bioteknolojia ya Kisasa.
Itifaki
hiyo pamoja na mambo mengine inasisitiza nchi wanachama kuandaa Sheria na
kuweka mfumo na mwongozo wa Usimamizi salama wa Mazingira na kulinda afya ya
binadamu, bioanuai na wanyama
Aidha, lengo la teknolojia ya Kisasa ni kukidhi haja ya
kuimarisha ubora, kudhibiti magonjwa, kuhimili ukame na kukuza uzalishaji. Hata
hivyo imebainika kuwa bado kuna wasiwasi wa athari zinazoweza kupatikana
kutokana na teknolojia hiyo endapo itatumiwa bila kufuata utaratibu. “kwa hiyo
tumewaita ili kujadili na kutoa maoni kuhusu utekelezaji wa Kanuni hizi ili
tupate mwelekeo wa suala hili na kuishauri Serikali’. Alisisitiza Eng. Mwihava.
Akitoa maezo ya awali, Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira,
Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Julius Ningu amesema kuwa lengo la kanuni hizo si
kuzuia au kukwamisha matumizi ya Bioteknojia hapa nchini bali ni kuhakikisha
nchi inanufaika na matumizi hayo kwa kuzingatia usalama wa afya ya binadamu na
Mazingira.
Aidha baadhi ya wadau katika kikao hicho walikuwa na maoni
tofauti na kuitaka Serikali kupitia upya kanuni na kufanya tathmini ya kuondoa
ama kuacha kuondoa kipengele cha Strict
liability.
Mkutano huo umehusisha wanasheria, wanasayansi, Mtandao wa
wawakilishi wa wakulima na Taasisi za Utafiti za Mbegu, hususan Pamba na
Mahindi.
No comments:
Post a Comment