![]() |
| Bondia Lucas Ndula wa Muheza kushoto akioneshana uwezo wa kuoneshana uwezo wa kutupiana masumbwi na Iddy Mkwera wa Dar es salaam katika uwanja wa jitegemee muheza wakati wa sikukuu ya Pasaka Mkwera picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com |
![]() |
| Bondia Iddy Mkwera akinyooshwa mkono juu baada ya kumgalagaza Lucas Ndula wakati wa mpambano wa mabondia wa Dar na Muheza Mkwera alishinda kwa pointi mpambano hou wa raundi sita uliotahalishwa kwa ajili ya kuinua mchezo wa ngumi Wilaya ya Muheza na kusherekea sikukuu ya Pasaka picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com Na Mwandishi Wetu Bondia Iddy Mkwera wa Dar es salaam ameibuka mshindi baada ya kumgalagaza bondia Lucass Ndula wa Muheza wakati wa mpambano wa kuhamasisha masumbwi Wilayani Muheza uliochezwa wakati wa sikuku ya Pasaka katika uwanja wa Jitegemee Mpambano ulioanza kwa ndula kuanza kwa kasi na kushangiliwa na wapenzi wengi katika raundi ya kwanza na ya pili upepo ulianza kumbadilikia raundi ya tatu baada ya kukata pumzi uku akitupa ngumi bila mpangilio wakati Mkwera akipanga mashambulizi na kupiga ngumi kali za kushitukiza zilizo mfanya Ndula kutulia Raundi ya tano ilikuwa ni mfululizo wa makonde yaliyorushwa na Mkwera kwa ajili ya kumuhadhibu ndula ilipofika raundi ya sita na ya mwisho wa mchenzo ndula alipigwa upcat ambayo ilimchanganya na kufanya kuwa nje ya mchezo kwa kushika magoti ambapo aliokolewa na kengele iliyoashilia kumaliza mpambano huo wa raundi sita na kufanya Iddy Mkwera kuibuka na ushindi wa point akipeperusha vema bendera ya Dar es salaam katika wilaya ya Muheza Mfadhili wa mpambano huo ambaye aliwezesha kila kitu ikiwemo kupereka mabondia kutoka Dar pamoja na ulingo maarumu kwa ajili ya masumbwi Allan Augastino ame haidi kurudia kufanya onesho hilo la wazi katika viwanja hivyo hivyo vya Jitegemee Muheza mkoa wa tanga wakati wa sikukuu ya Iddi na kuwataka wapenzi kujitokeza kwa wiki Mpambano huo uliofanyika katika katika viwanja vya wazi vya Jitegemee iliwavuta wapenzi wengi wakiwemo watoto ,wanawake na vijana mbalimbali waliojitokeza kwa wingi |


No comments:
Post a Comment