Kuingia katika siasa
Baada ya kumaliza masomo alishughulika hasa na biashara za familia alizorithi kutoka kwa babake.Wengi walitarajia kuwa angeshinda lakini baada ya kushindwa , Uhuru alighadhabika sana na hata kuahidi kuasi siasa.
Wengi waliona hatua ya Moi kama kumtayarisha Uhuru kwa mambo makubwa katika siku za baadaye
1999 Rais Daniel arap Moi alimpa cheo cha mwenyekiti wa bodi ya utalii. Moi aliendelea kumpandisha ngazi kwa kumpa nafasi ya mbunge mteule na kumfanya waziri msaidizi.
2002 akawa makamu mwenyekiti wa KANU. Chama cha KANU kuanzai ahpo kikaanza kugawanyika huku vigogo wa chama hicho wakiondoka chamani.
Tangu alipoingia katika ulingo wa Moi, Uhuru amekwa akitaka kuonyesha watu kuwa yeye anaweza kujitegmea mwenyewe wala sio kibaraka cha Moi kama wengi walivyokuwa wanasema. Baadaye alimshinda kigogo wa chama cha KANU Nicholas Biwot walipogombea uwenyekiti wa chama hicho
Mgombea wa urais 2002
Tangu Julai 2002 ilionekana wazi ya kwamba Moi alimtaka kama mgombea wa urais upande wa KANU atakayemfuata katika ikulu. Mkutano mkuu wa KANU katika mwezi wa Oktoba 2002 uliitikia mapenzi ya rais ukamtangaza Uhuru kama mgombea wa urais.Tendo hili lilisikitisha wanasiasa wengi wasiokuwa Wakikuyu na kutegemea nafasi hii kwa ajili yao wenyewe. Waliondoka katika KANU na kuendelea katika ushirikiano wa upinzani wa NARC.
Kiongozi wa upinzani na wa chama
Katika bunge jipya alikuwa kiongozi wa upinzani lakini aliona pia upinzani ndani ya chama hasa kutoka kwa Nicholas Biwott pamoja na wanasiasa kutoka Bonde la Ufa.Kwenye mkutano wa chama cha Januari 2005 Uhuru alithibitishwa kwa kura nyingi na hapo Biwott akodnoka chamani na kuunda chama chake cha New Kanu.
Upingamizi dhidi yake ndani ya KANU
Katika kura maalumu ya wananchi kuhusu katiba mpya Uhuru alishikamana na viongozi wengine katika kambi ya machungwa.Mipango yake ya kushiriki katika Orange Democratic Movement(ODM) yalipingwa vikali ndani ya chama kwa sababu wana KANU pamoja na rais mstaafu Moi waliogopa kupotea kwa chama cha kwanza katika historia ya Kenya.
Katika Novemba 2006 Biwott alirudia jaribio la kumpindua Uhuru kwa kuita mkutano wa Kanu mjini Mombasa bila idhini ya mwenyekiti wala kamati ya chama.
Uhuru alipinga na mahakama kuu ikabatilisha kura ya Mombasa tar. 29 Desemba 2006 ikathibitisha azimio hili katika Juni 2007.
Kuhamia upande wa Kibaki 2007
Juni 2007 Uhuru alionyesha wazi ya kwamba alitaka kuacha ushirikiano wa ODM kwa kutopeleka jina lake kati ya wagombea wa urais upande wa ODM. Badala yake alieleza ya kuwa atampigania rais Kibaki achaguliwe tena. Alisema hana nia ya kugombea urais ikiwa hana uhakika kuwa atashinda.Kufuatia uchaguzi uliokumbwa na utata, Kibaki alitawazwa kama rais licha ya utata huo. Kibaki naye alimteua Uhuru kama waziri wa serikali za mitaa na baada ya mapataono kati ya Kibaki na Odinga , Uhuru aliteuliwa kama naibu waziri mkuu ikiwa ni sehemu ya kugawana mamlaka.
Kenyatta ameweza kuchaguliwa kama rais baada ya kumshinda mpinzani wake Raila Odinga kwa idadi ya kura za urais na kupata asilimia hamini nukta tatu , kama inavyohitajika na katiba mpya.
No comments:
Post a Comment