header

nmb

nmb

Friday, March 1, 2013

Wafanyakazi kunufaika na mkataba wa hali bora


Katibu wa chama cha wafanyakazi wa hifadhi, mahoteli, majumbani, huduma za jamii na ushauri Mfumu Silvester akiongea na mtandao huu ofisini kwake leo.


Na Gustav Chahe, Iringa

CHAMA cha wafanyakazi wa hifadhi, mahoteli, majumbani, huduma za jamii na ushauri (CHODAWU) kimeanza mkakati wa mikataba ya hali bora na mishahara kwa wanfanyakazi ili kuinua hali zao kimaisha.

Akizungumza na mtandao huu ofisini kwake leo Katibu wa chama hicho Mkoa wa Iringa Mfumu Silvester alisema chama kimefikia uamuzi huo kutokana na hali ngumu ya maisha na kupanda kwa gharama za maisha kutokana na mishahara yao kutokukidhi haja.

Amesema chma kinaanza kukutana na waajiri kwa ajili ya kujadili na kusaini mikataba hiyo kwa ajili ya kuwawezesha wafanyakazi wao kufanya kazi kwa moyo na kwa bidii.

“Kwa kuwa mikataba ya hali bora ya wafanyakazi imeshaandaliwa, tunataka kukutana na waajiri ili tuweze kujadili na kusaini ili ianze kutumika mara moja katika mwaka wa fedha na serikali unaoanza Julai Mosi, Mwaka huu” amesema Mfumu.

Amesema Mkoa wa Iringa pekee una taasisi nyingi ambazo ni wanachama wa chama cha wafanyakazi cha Chodawu ambao wanalengwa kunufaika na mkataba huo.

Pia amesema taasisi hizo ni pamoja na hifadhi kwa Camp Site zinazoshughulika na utalii ndani ya hifadhi ya Ruaha ya Mkoa wa Iringa.

Ili kufanikisha hilo, amewataka wale wote ambao hawajajiunga na Chodawu, wajiunge haraka ili wakati mikataba hiyo inaposainiwa waweze kujumuisha kwa kuanza kunufaika nayo.

Amefafanua kuwa wanaohusika na mkataba huo ni Hoteli zote, Lodge, Petro station, Super Market, Shule za private, walinzi binafsi (security guard), Wafanyakazi wa Taasisi za dini (R.C, K.K.K.T, Anglican) na waajiriwa wa ofisi za vyama vya siasa na taasisi za huduma kwa jamii (NGOs).

“Kazi ya Chodawu ni kuhakikisha kunakuwa na mahusiono na wajibu baina ya mfanyakazi na mwajiri inatekelezwa inatekelezwa kulingana na sheria namba 6 ya ajira na mahusianao ya mwaka 2004” amesema.

Chama cha wafanyakazi (Chodawu) lianzishwa chini ya sheria ya usajili wa vyama vya wafanyakazi kifungu cha 8 cha sheria ya mwaka 1998

No comments:

Post a Comment