header

nmb

nmb

Thursday, March 28, 2013

PRECISION AIR YAANZA KUKEA WADAU HATARINI KUKWEPWA!!


Kaka Lukaza, tafadhali naomba uniwekee hii post, usinibanie. Siku ya Jumamosi (23 Machi 2013) nilikuwa na safari ya kutoka Arusha kurudi Dar es Salaam kwa kutumia usafiri wa ndege wenye ‘jina kubwa’ hapa Tanzania, Precision Air! Kama unavyofahamu, siku hizi wana-flight za moja kwa moja kutokea Arusha Airport kwahiyo nilikuwa sina wasi wa kupanda shuttle mpaka KIA ili kuweza kurudi kwa familia yangu Dar es Salaam.

Mimi na abiria wenzangu tulitakiwa kuondoka Arusha saa 7 na dakika 20, kumbuka tangia saa 4:45 tulikuwa airport kwa kukamilisha utaratibu wa check-in time. Kwenye saa 6 mchana tuliambiwa tukafanyiwe ukaguzi wa mwisho wa usalama kabla ya kuondoka lakini cha kushangaza baada ya nusu saa kuna mfanyakazi mmoja wa shirika hilo aliyejitokeza na kwa bila kutumia lugha ya staha alituamrisha kuwa sasa tumebakia na option mbili; kupitia Zanzibar au kusafirishwa hadi KIA nakuwahi ndege inayofuata kuelekea majumbani kwetu Dar es Salaam. BILA HATA KUTOA SABABU AMA KUTUOMBA RADHI! Abiria tuliwaka kweli kweli! Hapo tumeshachoka, tunanjaa, na hako kajamaa hata hakataki kutusikiliza!

Anyways, Precision Air waliweza kuruhusu abiria kama 10 kupitia Zanzibar – Nairobi – Dar es Salaam (ambayo hata hivyo sijui kama walifika saa ngapi), huku sisi masalia wengine kama 25 hivi tukapandishwa kwenye mkweche wa basi kuelekea KIA (picha nimeambatanisha hapo kwenye email). Hapo hapo sisi tuliopandishwa kwenye hiyo basi iliyochoka na kutoa harufu kweli kweli hatukuambiwa hata hiyo ndege tutakayoenda kuipanda KIA inafika na kuondoka saa ngapi. Ni cha kushangaza sana kwamba mfanyakazi wa Precision Air aliyetuamrisha kwenda KIA alikuwa hana majibu haya!

Ndugu zangu, tumefika KIA bado tukakuta bonge la foleeeeni linatusubiria mpaka kufika ticketing counter! Huku tukiambulia machungu ya safari maana mpaka sasa hakuna mtu aliyetuomba radhi (kumbe makubwa zaidi yalikuwa mbioni kujitokeza)! Tumefika counter kwa nguvu zote ndo tunapewa taarifa kwamba ndege inayofuata inaondoka saa 2 na dakika 20 USIKU! Ambayo nayo ilipata delay mpaka saa 4 zaa USIKU! YAANI NIKAJIKUTA NIMEFIKA NYUMBANI SAA 6 ZA USIKU! UCHOVU, NJAA NA BADO SIJAOMBWA RADHI!!!

Maskini pia kuna wazungu wa watu ambao walikuwa wana International flight hiyo saa 4 usiku nao wakaponzwa na huu uzembe wa Precision Air!!! Embu angalia jinsi ilivyoweza kutzalilisha kitaifa pia!

Jamani wadau, Precision Air sio ndege yakupanda!!! Kama mnasafari zenu ni bora mkachungulie ndege zingine..bahati mbaya ushindani kwetu si sana ndo maana hata hii shirika la ndege inajitia kiburi kiasi hiki!!!

Kwangu mi binafsi sitapanda tena ndege ya Precision Air!! Nikikosa ndege ingine ni bora nikapande basi..ntajipangilia mi muda wangu binafsi wa kufika.

Kama Precision Air hawataweza kujirekebisha ni bora wakaifunga hiyo biashara, maana ni dhahiri kwamba hawaiwezi

No comments:

Post a Comment