Kinyang'anyiro ni kikali kati ya Muungano wa Cord na Jubilee wa Raila Odinga na Uhuru Kenyatta.
Kwenye ukurasa huu tutakupasha matukio kila yanapojiri hadi upigaji kura utakapokamilika mwendo wa saa kumi na moja jioni.
Unaweza kututumia maoni yako kuhusu uchaguzi kwenye ukurasa wetu wa Bofya facebook
11:25 Mkuu wa Polisi David Kimaiyo asema kuwa takriban wanachama 200 wa kundi la MRC au Mombasa Republican Council walivamia kituo cha polisi wa doria wakiwa wanaelekea kusambaratisha shughuli za kupiga kura. Inaarifiwa polisi wanne waliuawa katika makabiliano kati yao na wanachama hao.
11:14 Mgombea wa urais Uhuru Kenyatta anapiga kura yake katika eneo bunge lake la Gatundu , mkoa wa Kati
10:31 Mwandishi wa BBC mjini Eldoret Wanyama wa Chebusire vituo vilifungua mapema mambo, yameenda shwari kwa ujumla wake, lakini katika baadhi ya vituo, kumekuwa na mushkil , mashine ziligoma katika kituo cha kupigia kura cha shule ya msingi ya UG, zaidi ya wapiga kura elfu tatu , hadi sasa ni chini ya watu hamsini wamepiga
10:27 Mkuu wa tume huru ya uchaguzi Isaac Hassan anahutubia waandishi wa habari kuhusu changamoto inazokabiliwa nazo tyume hiyo. Isaac anasema vituo vilivyofungua kuchelewa, vitahakikisha wapiga kura wote wamepiga kura
10:22: Ingawaje tume ya uchaguzi IEBC inawakubalia watu wawasindikize wazee au wagonjwa kupiga kura, wapigaji kura wengine wanawakataza kufanya hivyo. Mjini Kisumu katika kituo cha upigaji kura cha Ukumbi wa Aga Khan, mwandishi wetu Ann Mawathe dada mmoja alieyejipandikiza blanketi tumboni ili kuwahadaa watu na akubaliwe kwenda hadi mwanzo wa foleni, alikatazwa kufanya hivyo na wapiga kura wenzake.
Katika kituo hicho hicho, baba fulani aliyekuwa amebeba kipochi cha mkewe aliyekuwa na mtoto mgongoni, naye alirudishwa hadi nyuma kabisa ya foleni hiyo. Pia, mwanamume mwingine aliyejitwika ufahari fulani kwa vile alikuwa kavalia suti, na kutaka kuruka foleni, alikatazwa kufanya hivyo.
08:43 Mgombea wa urais wa muungano wa CORD, waiziri mkuu Raila Odinga anatarajiwa kupiga kura yake wakati wowote kuanzia sasa
08:30Solomon Mugera anasema kwamba kupiga kura kunachukua takriban dakika 12
08:25 Hassan Majid pia mwandishi wa BBC anasema kuwa polisi wamepata mwili mmoja wa mtu aliyeuawa na mwingine kujeruhiwa kwa kukatwa panga katika eneo la Mishomoroni
08:24 Mwandishi wa BBC mjini Mombasa, Karen Allen anasema kuwa polisi wamepata maiti za polisi wanne ambao wameuawa katika eneo la eneo la Changamwe , Kaskazini mwa Mombasa. Hana taarifa zaidi kwa sasa
08:15:Fatma Sanbur yuko mtaani Kibera na anasema watu ni wengi sana lakini hakuna mbinu ya kupanga foleni. Anasema watu wanapangwa kwa orodha ya majina na hata baada ya saa moja tangu waanza kupangga foleni saa kumi na moja, shughuli ya upigaji kura ilikuwa haijaanza
07:11James Mwangi: Kwenye ukurasa wa Bofya Facebook wa Bofya bbcswahili anasema yuko kwenye foleni na habanduki
07:14 Hison Nyakundi : Yuko mjini Eldoret kwa Foleni tayari kupiga kura Bofya bbcswahili
07:24 Kips Oscar: Kupitia Bofya Facebook yuko katika kaunti ya Marsabit anasema upigaji kura unaendelea bila wasiwasi na kuwa wanatarajia shughuli itakamilika kwa muda bila wasiwasi
07:32: William Ruto anasema kuwa anajivunia uchaguzi wa Kenya unafanyika kwa amani licha ya dukuduku la wengi. Anasema anawataka wapinzani kukubali matokeo ya uchaguzi vyovyote matokeo hayo yatakavyokuwa.
07:43 Upiga kura bado haujaanza katika baadhi ya sehemu za Kenya. Wapiga kura wanalalamika kuwa katika vituo kadhaa tarakilishi zimegoma na kwa hivyo watasubiri muda kabla ya kupiga kura zao
07:47Eco Seyar Papa akiwa mjini Nairobi anasema Wakenya wamejitokeza kwawingi jijini Nairobi katika eneo la Dagoreti. Foleni zilianza kupigwa kuanzia saa tisa usiku tangu kuanzishwa kwa demokirasia ncini Kenya watu waeneo hili hawajawai kujitokeza kwa mapenzi kama inavyo onekana.
07:50 Mwandishi wa BBC Ann Mawathe yuko mjini Kisumu na anasema ameona foleni ndefu sana watu wakiwa hamasa kupiga kura. Wamepiga foleni tangu saa nane usiku.
07:52 Mombasa eneo la Kaloleni mpiga kura mmoja amesema hadi kufikia sasa upigaji kura haujaanza kwani maafisa wa tume ya uchaguzi bado hawajawasili na vifaa vyao
No comments:
Post a Comment