Wakati matokeo ya uchaguzi mkuu wa kidemokrasia nchini Kenya yakiendelea kuhesabiwa taarifa kutoka nchini humo zinadai kuwa Mgombea wa chama cha Jubilee Uhuru Kenyatta anaongoza kwa 52% na Raila Odinga ana 32%,
Uhuru ameendelea kung'ara zaidi kutokana na matokeo hayo kuendelea kumpa nafasi kubwa ya kushinda huku wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanadai kuwa umaarufu wake umetokana na vikwazo vya kesi iliyopo mbele yake japo wanadai upo uwezekano mkubwa wa kuibuka mshindi kutokana na hali halisi ya matokeo haya jinsi yanavyoendelea kumpa nafasi ya kuongoza .
Mbali ya Uhuru wa chama cha TNA kuongoza kwa kura 414, 973 ila bado mpinzani wake mkubwa katika kinyang'anyiro hicho Raila Odinga ( ODM) ambaye alikuwa anapata mashabiki lukuki katika kampeni zake yeye ana kura 279,773, huku anayeshika nafasi ya tatu ikishikwa na Musalia Mudavadi (UDF) 16, 355.
Katika matokeo hayo wagombea wengine wanaonyesha kufeli vibaya baada ya kuonekana kutupwa kwa mbali na wagombea hao watatu .
No comments:
Post a Comment