Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Balozi Christopher Mvula kushoto akizungumza na Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii ya Tanzania TTB Dk. Aloyce Nzuki wakati yeye na ujumbe wake walipomtembelea Mh. Balozi na kuzungumza naye mambo mbalimbali ukiwemo mkakati wa bodi hiyo katika kutangaza utalii wa Tanzania kupitia balozi zetu nchi mbalimbali za ulaya hasa maajabu matatu yaliyotangazwa juzi na taasisi ya Seven Natural Wonders ya Marekani ambayo ni Mlima Kilimanjaro, Mbunga ya Serengeti na Ngorongoro Crates, Bodi ya Utalii Tanzania TTB iko jijini Berlin nchini Ujerumani ikiongoza makampuni zaidi ya 43 ya utalii katika maonyesho ya kimataifa ya ITB yanayofanyika katika jengo la Mense Berlin.
Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB Dk. Aloyce Nzuki akitoa maelezo kwa Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Balozi Christopher Mvula kulia ni Msaidizi wa Kaimu Balozi Mama Maria Kejo jKutoka kushoto ni Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Balozi Christopher Mvula, Msaidizi wa Kaimu Balozi mama Maria Kejo, Mkurugenzi wa Masoko kampuni ya Bobby Tours na Mkuu wa utawala ubalozi hapo Bw. Adolf Mchemwa wakiwa katikamkutano huo janaKutoka kushoto ni Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Balozi Christopher Mvula akiandika mambo muhimu wakati Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB akielezea mkakati wa kuutangaza utalii wa Tanzania kupitia balozi zetu duniani kote kushoto ni Mkuu wa Masoko wa bodi hiyo Bw. Geofrey Meena
Hili ndilo jengo la Ubalozi wa Tanzania nchini Ujerumani jijini Berlin. Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania Dk. Aloyce Nzuki katikati akiwa pamoja na Meneja Mkuu wa Masoko wa bodi hiyo Geofrey Meena wakiwa nje ya ubalozi wa Tanzania nchini Ujerumani kulia ni Kassim Abdallah Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bobby Tours Mmoja wa maafisa wa ubalozi huo akiukaribisha ujumbe wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB ulioongozwa na Mkurugenzi wake Dk. Aloyce Nzuku kulia na Mkuu wa Masoko wa Bodi hiyo Bw. Geofrey Meena katikati ni Kassim Abdallah Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya Bobby Tours Kamimu Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Balozi Christopher Mvula akipokea majarida na DVD zenye mkakati wa kutangaza utalii wa Tanzania katika nchi za jumuiya ya Ulaya kutoka kwa Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB Dk. Aloyce Nzuki, mara baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika kwenye ubalozi wa Tanzania nchini Ujerumani jana, kushoto ni Mkuu wa Masoko wa TTB Geofrey Meena na kulia ni Msaidizi wa Kaimu Balozi Bi, Maria Kejo Kamimu Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Balozi Christopher Mvula na Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB Dk. Aloyce Nzuki wakiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa bodi ya utalii na maafisa wa ubalozi mara baada ya mazungumzo hayo xHili ndilo banda la Tanzania katika maonyesho hayo likiwa katika hatua za mwisho za kukamilika jana kabla ya kufunguliwa rasmi kwa maonyesho hayo leo Mkuu wa Msoko wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB Bw. Geofrey Meena akimueleza jambo Dk. Aloyce Nzuki
No comments:
Post a Comment